Monday, June 30, 2014

Aibu! Mwanamke amnasa KIKONGWE anayemtuhumu kumweka mwanaye ‘MSUKULE’ huko Mbagala

By on 7:08 AM

ULOZI! Katika hali ya kushangaza, mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika kwa jina moja la Siberi akiwa na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili lililotikisa, akimtuhumu kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara ‘msukule’.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina wakimhusisha kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.
Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
...Hii ni nyumba ya kikongwe huyo iliyoko maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar.
…Hii ni nyumba ya kikongwe huyo iliyoko maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.

CREDIT:GPL
  <<<KWA HABARI KILA SIKU BFYA HAPA ULIKE PAGE>>

0 comments:

Post a Comment