Sunday, July 6, 2014

MASHAMBULIO YAUA 30

By on 4:15 AM

Magari yaliyochomwa katika shambulio la Mpeketoni, Juni mwaka huu.
WATU 30 wamepoteza maisha katika mashambulio mawili tofauti huko Pwani ya Kenya karibu na mpaka wa Somali.
Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya imethibitisha kutokea tukio hilo.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku wengine wakiuawa kufuatia ufyatulianaji wa risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunti ya Lamu karibu na mpaka wa Somali.
Inadaiwa kuwa watu waliofariki walikuwa wakiangalia michuano ya kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa katika mashambulio mwezi uliopita.
Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.

0 comments:

Post a Comment