Showing posts with label HABARI ZA NJE. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA NJE. Show all posts

Sunday, August 17, 2014

REPORTED INFORMATION ABOUT EBOLA IN NIGERIA

By on 7:13 AM
EBOLA MIRACLE: Nigerian doctor survives …Discharged 2
BY AZOMA CHIKWE AND JOB OSAZUWA ON AUGUST 17, 2014 · COVER
■ Four others almost fully recovered –Health Minister
The first Nigerian who tested posi­tive to Ebola Virus Disease (EVD) has recovered from the virus and consequently been certified fit and dis­charged, the Minister of Health, Prof Onyebuchi Chukwu told newsmen yesterday in Lagos.
She was one of the doc­tors who had primary contact with the late Liberian Patrick Sawyer while attending to the deceased. Recall that people who had primary contact with late Sawyer, including medics at First Consultant Hospital, Lagos were quar­antined immediately Sawyer tested positive to Ebola virus infection.
The Minister explained that the medical experts at the isolation centre where she was admitted alongside others, have medically monitored the patient, and having fully sat­isfied with her recovery then discharged her home.
“The doctor is safe and free with no risk of infecting oth­ers and had been discharged to go back to her family. In fact, She is even safer than most people on the street who may not know that they have one symptom or the other. Her immunity is boosted and she was closely monitored before being discharged. The experts would have dis­charged her all this while but had to observe her very well because of the nature of the disease,” the Minister said.
He also said that four oth­ers similarly under medical management at the isolation centre were now almost fully recovered from the disease. He also said the other 189 persons, who had secondary contact, were still under sur­veillance in Lagos while ad­ditional six are in Enugu.
Towards arresting fur­ther spread of the disease, the Minister disclosed that patients under treatment were moved to the new 40-bed capacity isolation ward provided by the Lagos State Government at Mainland Hospital, Yaba.
However, the experimen­tal drug, Nano Silver, could not meet the requirements of the National Health Research Ethics Code. Consequently, the National Health Research Ethics Committee withheld approval for it.
Chukwu stated that the experimental drug was made available to the Emergency Operation Centre in Lagos, but was not administered to any patient while awaiting clearance by the Committee.
“However, Chukwu add­ed, “other candidate drugs are currently being evaluated by the Treatment Research Group for EVD. As soon as any of the experimental drugs is cleared by the Committee and is made available, we shall use it in the treatment re­gime subject to the informed consent of the patient.”
So far, out of the 12 people who tested positive, he said four people have died from the dreaded disease.
On the sack of resident doctors, Chukwu confirmed that the suspension is only temporal and that the Federal Government is considering how it can further improve the health care sector.
“I believe the suspension is only temporary, the govern­ment is looking at how the health care system can be im­proved. But please note that the suspension affects only federal-owned hospitals, it is not extended to other state hospitals.”
Recall that that there had been allegations by doctors that the health insurance scheme offered by the federal government had not yet been put in place. The doctors also alleged that health worker who volunteered had not been provided with health in­surance cover by the Federal Government.
Responding to this al­legation, Prof Chukwu ac­knowledged that the Federal Government had indeed not commenced the provisions of insurance policy cover but noted that the Lagos State government has started is­suing the insurance policy to doctors in its employ.
“We are still working on the paper works; when it is ready we would definitely give it out. But we still need more volunteers as health workers are little and they can’t handle the job alone,” he said.
he insurance policy to doctors in its employ.

Ni MaajabU Na Kweli.. Huyu ndiye Baba wa Familia aliyepata ujauzito na kujifungua

By on 6:47 AM
Familia inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata ujauzito na kujifungua.

Iko hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume alilokuwa nalo.

Hali ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa, yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili.

Wawili hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi kama mwanamke kamili akiihudumia familia yake na kuvaa mavazi ya kike kama mama siku zote.

Lakini kwa mujibu wa Bianca, wawili hao wamekuwa wakishiriki tendo la ndoa kama kawaida kwa kuwa wanaamini kubadili kwao mfumo wa maisha hakuwezi kubadili viungo vyao vya mwili. Matokeo yake, baba alipata ujauzito na kujifungua. Na hivi sasa wana watoto wawili.

Cha kushangaza ni kwamba wana ndoa hao hawawachanganyi majirani tu, lakini pia wamewaficha hadi watoto wao wadogo ambao wanaamini kabisa kuwa Bianca ndiye aliyewazaa na baba yao ni Nick. Lakini siri hii itakaa hadi lini ili hali majirani wanajua na wa wanandoa hao wameshaeleza kwenye vyombo vya habari?

“Sifahamu lini tutaanza kuwaambia ukweli, labda wakati ambapo Kai (mtoto wao mkubwa) atakapokuwa na miaka sita hivi, lakini wanatakiwa kuwa na umri mkubwa wa kutosha kuelewa. Ni muhimu wakifahamu kwa kuwa ni siri kubwa ya kuwaficha watoto wako na kama wakifahamu kupitia njia nyingine watachukia sana.” Alisema Bianca.


Biana aliendelea kujitetea kuwa kuwa jike dume/ dume jike haielezi jinsi ulivyo. Ni kama kuwa na rangi nyeupe, nyeusi, mnene au mwembamba haielezi kitu kuhusu jinsi ulivyo.

Kwa upande wa Nick, anasema mara ya kwanza alipopata ujauzito wa Kai alibadilika na kuishi kama mwanamke, hivyo ikawa kama yeye na mumewe wote ni wanawake. Wengi walidhani wanacheza mchezo wa kusagana.

Lakini alipopata ujauzito wa pili ndipo alipoamua kuishi maisha yake ya kawaida kama baba na kitumbo chake. Hali ilimnyima raha mbele za watu waliokuwa wanamshangaa sana.

“Lakini, nilipokuwa na ujauzito wa Pax (mtoto wa pili), watu walikuwa wananishangaa sana, kitu kilichonifanya nikose ujasiri. Sikuweza kuvumilia hali ile, watu kunong’onezana wakiniona, kuninyooshea video na mwisho nikawa siwezi kutoka nyumbani. Nilitoka kwenda kumuona daktari tu. Watu waliogopa kile wasichokifahamu.” Alisema Nick.

Naye Biance alipoulizwa kuhusu suala la kufanya mapenzi, hakusita kueleza wanavyoichukulia.

“Tunaviungo vyote kwa hiyo tunavitumia. Kama tungeweza kuvibadili tungefanya hivyo, ni ingekuwa tofauti- lakini hatuwezi na watoto wanakuja kwanza.”

Sasa hii tunaiitaje? Kila mmoja anatafsiri yake, kwa imani yake na uelewa wake pamoja na mila na desturi. Maajabu hayaishi! kwa lugha ya kiingerza tunaiita category ya Life Styl

Saturday, August 16, 2014

Ndege ya India iliyokuwa na abiria 280 yashuka futi 5000 angani baada ya rubani kusinzia

By on 12:59 AM

Mamlaka ya anga nchini India inachunguza tukio la hatari lililotokea Agosti 8, baada ya ndege ya Jet Airways Boeing 777-300 iliposhuka angani kwa zaidi ya futi 5000 (mita 1500) kutoka kwenye urefu waliopangiwa kuruka baada ya rubani wake kusinzia.
jet-airways
Tukio hilo lilitokea wakati ndege hiyo ikifanya safari kutoka Mumbai, India kwenda Brussels, Ubelgiji. Times of India imeripoti kuwa rubani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo alipumzika kidogo, mapumziko ambayo kwa viwango vya kimataifa huitwa ‘controlled rest’ kwa zile ndege za masafa marefu. Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Brussels ni masaa 9.
Rubani msaidizi alitakiwa kuchukua majukumu yote ya kuongoza ndege kwa wakati huo, lakini inadaiwa rubani huyo wa kike alisema naye alikuwa busy na tablet ya ndege hivyo hakugundua ndege ilipoanza kushuka kutoka kwenye urefu wa futi 34,000 iliyotakiwa kuruka wakati wanapita Uturuki.
Kwa bahati nzuri waongozaji wa anga wa Uturuki waligundua kuwa ndege hiyo iliyokuwa katika anga lao imeshuka kwenye urefu (altitude) ambao umepangwa kwaajili ya ndege nyingine, na kumtaarifu rubani msaidizi arudi kwenye urefu waliopangiwa.
Marubani wote wawili wa ndege hiyo wamesimamishwa kupisha uchunguzi .
Source: Aljazeera

Tuesday, July 8, 2014

BILIONEA WA LAKE OIL ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMTESA MFANYAKAZI WAKE

By on 6:11 AM


Mfanyakazi aliyeteswa.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni bilionea Ally Edha Awadhi ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kutokana na madai ya kumtesa mfanyakazi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari hii ofisini kwake wiki iliyopita, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar, ACP Jafari Mohamed Ibrahim aliyezungumza kwa niaba ya Kamanda wa kanda hiyo, CP Suleiman Kova alisema kwamba bilionea huyo na wafanyakazi wake wanaotuhumiwa kumteka, kumtesa na kumdhalilisha na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiusalama) walikamatwa na jeshi lake.
“Watuhumiwa wote walikamatwa hivi karibuni na kuhojiwa kisha wakapewa dhamana na upelelezi wetu umekamilika ambapo jalada hilo tumelipeleka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) lakini lilirudishwa polisi kwa sababu kulikuwa na upungufu, akaagiza lifanyiwe kazi tena,” alisema Kamanda Ibrahim.
Aliongeza kuwa baada ya jalada kurudi mikononi mwake alimtafuta mlalamikaji kwa njia ya simu akiwa Mwanza ili aje ahojiwe upya lakini hajaonekana hali iliyofanya alipeleke makao makuu ya jeshi la polisi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
“Ukitaka kupata habari zaidi nenda makao makuu ya polisi jalada la kesi hiyo liko huko,” alisema kamanda huyo.

Waandishi wetu walikwenda makao makuu ya jeshi hilo kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu (pichani), lakini wakaelekezwa kumuona msemaji wake, Advera Senso ambaye alisema upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.
Mlalamikaji wa kesi hiyo ambaye anadai kuteswa na kudhalilishwa aliamua kumwandikia barua ya malalamiko Waziri Mkuu Mizengo Pinda akidai kuwa mwenendo wa kesi yake hauendi vizuri hali iliyomfanya waziri mkuu aliagize jeshi la polisi kulifanyia kazi suala hilo ili haki itendeke.

Waandishi walienda ofisi ya waziri mkuu kutaka kujua kama kuna majibu ya agizo alilolitoa lakini cha kushangaza hakuna majibu yoyote yaliyopelekwa na jeshi la polisi kwa kiongozi huyo kwa mujibu wa maofisa wa ofisi hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Waziri Mkuu, Irene Bwire alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo, hakuwa na jibu la kuridhisha akaahidi  kulifuatilia ili kujua limefikia wapi.
Mlalamikaji huyo anadai kufanyiwa unyama huo Mei 2, mwaka jana na kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni lakini akadai hakuna kilichofanywa na jeshi hilo badala yake amekuwa akipata vitisho vya mauaji jambo linalomfanya aishi kwa kujificha.

Baadhi ya mambo aliyoyalalamikia mlalamikaji ni kupigwa na kujeruhiwa, kudhalilishwa na kudhulumiwa mali zake na mwajiri wake huyo.
Alizitaja baadhi ya mali hizo kuwa ni pamoja na nyumba, magari yake mawili ambayo ni Toyota lenye namba za usajili T 786 BZG na Toyota Fortuner namba T503 BQC, bastola, fedha taslim dola za Kimarekani 100,000, maduka na ofa zake tatu za viwanja huko Kigamboni.
Katika barua aliyompelekea waziri mkuu, mlalamikaji alidai kufanyiwa unyama huo na Awadhi kwa kushirikiana na mabaunsa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake katika chumba maalum wakimtuhumu kuiba dola za Kimarekani milioni 10.
 
CREDITS:GPL 
                          <<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE>>