Showing posts with label HABARI NA MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label HABARI NA MATUKIO. Show all posts

Friday, August 29, 2014

Ajinyonga shambani na kuacha ujumbe; “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”

By on 10:14 PM

Mtu mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema kijana huyo mwanamume amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Chalinze.
Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye maandishi hayo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu msaidizi, Athumani Mwambalaswa amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa na kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.
shambani
Hata hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa kijiji kipi kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta ndugu zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado hakijajulikana

SMS za Usagaji za Aunt Lulu Zanaswa…Zilikuwa zinaenda kwa binti wa kidato cha pili

By on 9:50 PM
Mama mmoja mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Zahara, ameibuka na madai mazito akimtuhumu msanii wa filamu ambaye pia ni mjasiriamali, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ kumtumia ‘SMS’ za usagaji mwanaye aitwaye Zahara  ambaye ni denti wa kidato cha pili.

MSIKIE MAMA MWENYEWE

Akizungumza kwa hasira, Mama Zahara aliwaka: “Mimi nina mtoto huyu tu wa kike, anasoma boarding huko Tanga lakini hivi karibuni alirejea akidai wamepewa likizo ya wiki moja.
 
“Tangu huyu mtoto amekwenda boarding, nimebaini amebadilika sana, amekuwa na vijitabia ambavyo sivielewi hivyo nikawa namchunguza sana.
 
“Leo (Jumanne wiki hii) wakati niko jikoni nikasikia anaongea na mtu akiwa chumbani kwake, mazungumzo yale yalinitia shaka kwani kuna muda nikamsikia ‘akimkisi’ aliyekuwa anazungumza naye.
Msanii wa filamu za Kibongo Lulu Mathias.
Msanii wa filamu za Kibongo Lulu Mathias.
“Nilihisi kitu f’lani lakini nikasema nitamvizia nichukue simu yake nikiamini kama kuna kinachoendelea nitagundua, na kweli, alipotoka kwenda bafuni nikaichukua simu yake na kukutana na mambo ya ajabu.
 
“Nilinasa hizi sms ambazo zilinionesha waziwazi kwamba mwanangu anafanya vitendo vya kisagaji. Niliumia sana hasa ukichukulia kwamba nina binti huyo tu.

“Nilipoichukua ile namba, nikataka kujua kama kweli alikuwa anachati na msichana mwenzake au mwanaume, ikabidi nifanye kama nataka kumtumia pesa kwenye simu yake na hapo ndipo likaja jina la Lulu Semagongo.
 
“Nilishtuka kwani namjua huyu msanii tangu alipokuwa mtangazaji. Nilipompigia akanijibu kwa kifupi tu kwamba nimlee vizuri mwanangu na yeye hawezi kumfanyia vitendo hivyo, nikaona bora nije kwenu mtanisaidia.”

MESEJI ZENYEWE ZIKOJE?

Zahara: Natamani kufanya kale kamchezo, unaweza kunisaidia?
Anti Lulu: Nitumie pesa!
Zahara: Kiasi gani cha pesa? Pesa siyo tatizo, umenielewa lakini? Nataka tu…(kitendo kichafu).
 
Anti Lulu: Nitumie hiyohiyo, kwa muda huu nitumie 30,000.
Zahara: Sawa halafu tunaonana vipi?
 
Anti Lulu: Nitumie pesa muda huu, Jumamosi.
Zahara: Mbona mbali sana mpenzi, leo haiwezekani au hata kesho, pesa siyo tatizo.
 
Anti Lulu: Nitumie pesa basi.
Zahara: Subiri kidogo baby, simu yenye pesa iko kwenye chaji, usijali, nashukuru kwa kunionea huruma.
Anti Lulu: (kimya).

KESHO YAKE

Anti Lulu: Umeona ishu kunidanganya siyo?
Zahara: Siwezi kukudanganya mpenzi, ndiyo naamka nitakutumia ila usije ukanidanganya maana nina…, hiyo Jumamosi tunaonana wapi?
 
Anti Lulu: Tuta-meet (kukutana) Bondeni Hotel (ipo Magomeni, Dar), basi nitumie hiyo pesa.
Zahara: Nikutumie kwenye namba hii, vipi tutatumia vifaa?
 
Anti Lulu: Nitumie kwenye namba hii.
Zahara: Nijibu basi kama tutatumia vifaa au hivihivi…
 
Anti Lulu: Hakuna haja ya vifaa, mimi natosha…
Zahara: Haya natuma, nitafurahi sana.
 
Baada ya maelezo ya mama huyo kisha kuziona sms hizo, kweli zilionesha Zahara ndiye aliyekuwa akimshawishi Anti Lulu amfanyie kamchezo hako huku msanii huyo naye akionesha kuujua na kutaka apewe kwanza Sh. 30,000, Ijumaa lilimsaka Anti Lulu ili kupata maelezo yake ambapo alikuwa na haya ya kusema:

HUYU HAPA ANTI LULU

“Kusema ukweli huyo binti ndiye aliyekuwa akinisumbua kwa kunitumia sms za kunitaka.
 
“Alionekana kuuzoea na kuupenda sana sana huo mchezo, mimi sijawahi, ni two different things (vitu viwili tofauti).
 
“Inavyoonekana alitaka kunichafua kwani alinilazimisha sana, sijawahi kufanya huo mchezo na wala sifikirii hasa kwa binti kama mimi ambaye naamini wapo wanaume wanaonipenda, niingie kwenye usagaji natafuta nini?

“Huyo binti mwambieni anikome kabisa.”
 
Chanzo: Gazeti la Ijumaa/gpl

Polisi amgonga mtoto, Aingia mitini na kutelekeza gari

By on 8:43 PM

Polisi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya  mkoani  Morogoro.
 
Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi alilishuhudia, mara tu baada ya kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na mihogo, askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake lililokuwa bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.
 
Wananchi waliojawa na hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari hilo na kutaka kulichoma moto, lakini busara za baadhi yao ziliwezesha kitendo hicho kutofanyika na baadaye trafiki alifika kudili na tatizo hilo
 
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina ya Toyota Baloon lenye namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto aliyegongwa alikuwa akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu kichwani.
  polisi1
Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti huyo alikuwa ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi wa pembeni gari hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha pikipiki.
polisi2
 
Hata hivyo, siku moja baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu aliyemgonga alikwenda hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa amefariki.

Sunday, August 17, 2014

JIWE Laporomoka jijini Mwanza na kuua Watu Wanne

By on 9:47 PM

Vilio na simanzi jana vilitawala kwa wakazi wa maeneo ya Sinai-Mabatini, baada ya vifo vya watu wanne wa familia mbili tofauti, vilivyotokana na mvua iliyosababisha miamba mikubwa ya mawe kuporomoka na kuponda nyumba zao usiku wa manane. 
 
Tukio hilo la kusikitisha limeripotiwa kutokea saa nane usiku kuamkia jana, wakati mvua   iliyoambatana na upepo wa wastani ilipokuwa ikiendelea kunyesha, na kusababisha miamba hiyo mikubwa inayokadiriwa kufikia tani mbili kuporomoka na kuziponda nyumba hizo na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wanne. 
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua.
 
Mpekuzi ilifanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia miamba hiyo ikiwa imeharibu nyumba, huku nyumba moja iliyojengwa kwa matofali ya tope ikiwa imeanguka na kubaki kifusi.
 
Nyumba zilizokumbwa na maafa hayo zinamilikiwa na watu waliotajwa kwa majina ya Joseph William na Lameck Ajiji, na kila moja watu wawili wamefariki kwa kukandamizwa na miamba hiyo.
jiwe1
 
Katika nyumba ya William iliyokuwa na watu watano, waliofariki wametajwa kuwa ni Kefa Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12), wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani na majeruhi mmoja ambaye hakufahamika jina lake ambaye alikimbizwa hospitali.
 
Nyumba inayomilikiwa na Ajiji yenye watu watatu, waliofariki wametambuliwa kuwa ni mama wa nyumba hiyo, Kwinta Geko (24) na mumewe Samson Odinya.
 
Waliojeruhiwa ni mtoto Bety Samson (4) na Godfrey Joseph (14) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani.
 
Tukio hilo ni la pili kutokea katika eneo hilo la Sinai. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya miamba kuporomoka na kusababisha vifo vya watu wawili wa familia moja.
 
Tukio la jana lilivuta hisia tofauti kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, huku wengine wakiangua vilio.
jiwe2
Mamia ya wananchi waliofika eneo hilo, walijitolea kwa kumpa fedha mtoto Bety aliyenusurika kufa kutokana na tukio hilo.
 
Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (Chadema), alifika eneo la tukio na kutoa pole kwa wananchi, ndugu jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionyesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyefika eneo hilo.
 
Akizungumza kwa kutumia kipaza sauti mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo la tukio, alisema: “Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa Serikali na mchana nitarudi hapa tena.”
 
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwandishi katika eneo la tukio, waliiomba Serikali kuzuia wananchi kujenga karibu na miamba mikubwa, kwani kufanya hivyo itasaidia sana kuepusha maafa kama hayo.
 
“Kwa kweli tukio hili linasikitisha sana, na tunaomba viongozi wa serikali wasaidie wananchi kuwaondosha kwenye maeneo ya kwenye miamba,” alisema mmoja wa wananchi hao ambaye pia ni balozi wa Shina Namba Tano, Mtaa wa Nyerere A, Jackson Kitundu.

JOHARI Amrushia Dongo IRENE UWOYA….Awachana Waigizaji wa Kike wanaojichia na Kupoteza Mvuto

By on 9:44 PM

Msanii  Johari Blandina ‘Chagula’ ambaye ni star mkongwe Swahiliwood amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuutunza muonekanio wake na kuwa kama kijana licha ya umri wake kuwa mkubwa tofauti na baadhi ya waigizaji wenzake wa kike ambao hujiachia na kuonekana wazee licha ya umri wao kuwa mdogo.

Akizungumza na Filamucentral Johari alisema:

“Wasanii wa kike wengi ni watoto wadogo lakini kwa sababu ya kujiachia wanaonekana kama watu wazima lakini ukweli ni watoto wadogo sana, namshukru Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini mwili wangu upo fiti,”
 
Johari alimtolea mfano Irene Uwoya ambaye ni shoga’ke wa karibu kuwa anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya kujiachia licha ya kwamba amempita miaka kadhaa. 
johari
 
Vile vile Johari amesema kuwa kawasasa amerudi kwa moto wa kasi kama muigizaji kama awali baada ya kuwa upande wa producer kuwapa nafasi chipukizi ambao wengi amesema wameshindwa, hivyo amerudi mwenyewe kwenye game.

Alikiba: Nawaomba watu Wasinikosanishe na Diamond, Sina Ugomvi Naye

By on 6:12 AM

Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.
alikiba

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.
Diamond Platinumz
Diamond Platinumz

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

Saturday, August 16, 2014

NDANI YA HABARI: Watoto 11 chumba kimoja, watumikishwa kuuza vitumbua

By on 12:07 AM
“Hao watoto hatujawaiba, tumewatoa kwao huko mikoani na biashara wanazofanya ni hizo ndogondogo wala siyo ngumu. Wengine hapa hawana baba wala mama wanazunguka tu mitaani. Wameona kuliko kuiba, ni bora waje wafanye kazi ili wapate pesa za kujikimu,” anasema Fatuma. 
Na Elias Msuya, Mwananchi

  • Mmiliki wa biashara hiyo asema alifanya hivyo kuwasaidia kwa kuwa wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.


Pengine takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) kwamba watoto wapatao milioni 250 wanatumikishwa katika ajira mbalimbali duniani kote, zikawa ndogo kulingana na hali halisi kwa kuwa kila kukicha, mapya huibuka.
Ajira hizi zinapaswa kupigwa vita kwa kuwa siyo tu zinawanyima haki za msingi watoto, bali zinachochea umaskini kwa familia na taifa kwa jumla.
Hassan Abdallah mkazi wa Tabata ni mmoja kati ya wanaoshiriki katika biashara hii haramu ya kuajiri watoto. Hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuajiri watoto 11 kwa kazi za kuuza vitumbua huku akiwahifadhi ndani ya chumba kimoja.
Kati ya waajiriwa hao, watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wako wanane.
Katika makazi hayo, watoto walimwonyesha mwandishi wa habari hizi banda la mabati wanalotumia kwa malazi likiwa kando ya nyumba ya mwajiri wao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisukuru, Lukresia Msuya anasema kuwa Abdallah na mkewe Fatuma Shomari wamekuwa wakiwafuata watoto hao mikoani na kuwaleta jijini Dar es Salaam kuwatumikisha kuuza vitumbua mitaani.
“Tulipigiwa simu juzi na katibu wa CCM wa mtaa akisema kuwa kuna jambo la muhimu. Hapo ndipo aliponionyesha nyumba hii ambayo ina watoto wanaotumikishwa kuuza vitumbua. Tukawakusanya na kuwapelekapolisi,” anasema Msuya.
Amewataja watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo kuwa ni pamoja na Furaha Samuel, Steven Tudius, Amani Adison, Yusuf Simon, Richard Zakaria, Kackson Jackson Michael, Elia Wilson, Boniface Lawrence, Baraka Francis, Zamda Yumpunju, Jema Ramadhani na Haji Ramadhani.
Msuya amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kisukuru kisha kuhamishia shauri hilo Stakishari ambako Abdallah aliwekwa ndani.
“Nikiwa kama mzazi inaniuma kuona watoto hawa wadogo wenye umri kati ya 17 na 12 wakifanyishwa kazi kama hizi. Nawaomba wazazi wawakumbatie watoto kama vifaranga vya kuku. Mtoto wa miaka 12 umfanyishe kazi, halafu utamlipa nini kama siyo kumdhulumu?” alihoji.
Jinsi walivyokamatwa
Akieleza jinsi alivyogundua suala hilo, katibu wa CCM wa Mtaa wa Kisukuru, Thomas Matiku anasema kuwa alipewa taarifa na wananchi wakati akitoka Buguruni.

Friday, August 15, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA: KIBANO! TRAFIKI WAMGUNGIA KZI DEREVA JEURI

By on 10:24 PM

Stori: Deogratius Mongela na gabriel ng’osha
DEREVA wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimdhibiti dereva wa basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) aliyevunja sheria ya usalama barabarani.
Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.
Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya 'trafiki'.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimtoa nje dereva jeuri wa UDA.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao,  mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi  Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.
Tunashauri madereva kuwa makini na watiifu pindi wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa zikitokana na uzembe wa madereva kwa kutotii sheria za usalama barabarani-Mhariri.
JIUNGE NA GURUDUMU KWA KULIKE PAGE

HABARI PICHA:AFANDE SELE AZIMIA AKIMZIKA MKEWE!

By on 10:22 PM

Stori: Dustan Shekidele,Morogoro
Mfalme wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameshindwa kustahimili msiba wa mkewe, Asha Msindi (34) na kujikuta akizimia msibani wakati wa maziko, Risasi Jumamosi lina stori ya kusikitisha.
Mwili wa marehemu Asha Mohamed Shiengo 'Mama Tunda' ukiombewa kabla ya mazishi.
Tukio hilo ambalo liliibua simanzi nzito mkoani hapa na kuweka historia lilijiri juzi, Alhamisi katika Mtaa wa Amani, Mji Mkuu, alipokuwa akiishi Asha na mama yake.
Aliyekuwa mke wa Afande Sele, Asha Msindienzi za uhai wake.
RAFIKI AFUNGUKA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Afande, gwiji huyo wa muziki ambaye alitengana na mkewe mapema mwaka huu, alipopewa taarifa hizo za msiba, hakuamini hadi alipofika nyumbani kwa marehemu na kukuta watu wamejaa msibani.
Mfalme wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ akiwa amezimia msibani.
“Alipigiwa simu na baadhi ya ndugu wa mke kumueleza habari za msiba, hakushtuka sana maana hakuwa ameamini moja kwa moja hivyo akasema ataamini atakapofika msibani na kukuta msiba,” alisema mtu huyo wa karibu ambaye aliomba hifadhi ya jina gazeti.
Afande Sele akiweka udongo kwenye kaburi la mke wake Mama Tunda.
AZIMIA
Mtu huyo wa karibu alizidi kueleza kuwa, mara baada ya kufika nyumbani hapo na kukuta ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika ndipo Afande alipoanguka na kuzimia kwa takriban saa nne kisha akaziduka.
“Alipofika pale nyumbani kwa mkewe na kukuta umati ukiwa msibani, alijitahidi akaingia ndani na alipomuona mama mkwe wake, hapohapo alianguka na  kuzimia,” alisema mtu huyo.
Mama wa marehemu Asha Msindi (34), Hamida Rajab Sulu.
APEPEWA
Rafiki huyo wa Afande alizidi kueleza kwamba, baada ya kuzimia, ndugu wa mke walimlaza kwenye kochi kisha baadaye rafiki zake walimchukua na kumpeleka nyumbani kwake maeneo ya Msufini ambapo walimpepea kisha wakammwagia maji ya baridi, akazinduka.
Alipozinduka, aliwaomba marafiki zake wampeleke tena msibani ambapo alipofika aliomba kuletewa mwanaye mdogo, Asantesanaa, akambeba na kukaa naye msibani hapo.
Majirani waliofika msibani wakiwa pamoja na mama wa marehemu(Asha Msindi), Hamida Rajab Sulu(wa kwanza kulia).
CHANZO CHA KIFO
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mzazi wa marehemu, Hamida Rajab Sulu, alisema kuwa mwanaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kali kwa takriban siku tatu, ndipo Jumatano iliyopita asubuhi walipompeleka katika Hospitali ya St. Mary mjini hapa.
Alisema kuwa alipofikishwa hospitalini hapa alilazwa na kuanzishiwa dozi ya malaria lakini baadaye hali ilizidi kuwa mbaya wakalazimika kumuhamishia kwenye Hospitali ya Manispaa ya Morogoro.
“Walimlaza pale kwa saa kadhaa, walipoona hali inazidi kuwa mbaya, walitushauri tumuhamishie kwenye Hospitali ya Manispaa Morogoro.“Tulipofika pale walimuanzishia dripu ya kutibu malaria, kabla hata haijaisha, mgonjwa alianza kutikisa miguu, hapohapo akafariki dunia. Ilikuwa muda wa saa 5:00 usiku,” alisema mama huyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba akimpa pole Afande Sele.
WASANII WATINGA MSIBANI
Msiba huo umeacha historia ya aina yake kwani kesho yake asubuhi (Alhamisi), wasanii wengi walifika msibani hapo kwa ajili ya kuomboleza hali ambayo iliwafanya baadhi ya watu kushangaa wasanii badala ya kuomboleza.
Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Mohammed Shiengo ‘Mama Tunda’ enzi za uhai wake, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.
Miongoni mwa wasanii ambao walifika mapema msibani hapo ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini, Simon Mwakifwamba na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.
AFANDE ANENA
Akizungumza kwa uchungu makaburini hapo, Afande Sele alisema kifo cha mkewe ni pigo kubwa maishani mwake kwani ndiye aliyekuwa faraja ya pekee kwa wanaye, Tunda na Asantesanaa.
“Hili ni pigo kubwa maishani mwangu, mama Tunda alikuwa ndiye kila kitu kwa wanangu, inaniuma sana,” alisema Afande akitokwa machozi.
Mwanamuziki Profesa Jay (kulia) akimfariji Afande Sele.
AZIKWA
Baada ya umati kujikusanya msibani hapo, taratibu za mazishi zilifanyika siku hiyohiyo na wakaelekea kuzika kwenye Makaburi ya Kola mjini hapa.
TUJIKUMBUSHE
Kabla Afande Sele na mama Tunda hawajatengana mapema mwaka huu, waliishi kama mume na mke kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata watoto wawili, Tunda na Asantesanaa.

Mrembo Amwagiwa Mafuta ya Moto Usoni kisa mume wa mtu

By on 9:07 AM

Mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema:

“Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana yake.
 
“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita kwake, nilikuwa sipajui ila akanielekeza, ile nafika tu majirani zake wakamwambia mimi ndiye nilikuwa nakwenda kulala pale na mume wake.
moto
“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto akanimwagia usoni.
 
 
“Nikaanza kupiga kelele, watu wakajaa  ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni hapahapa duniani.”
 
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja kuzungumzia tukio hilo.

Ugonjwa wa EBOLA Waingia Dar es Salaam……Wagonjwa wawili wagundulika kuwa nao

By on 9:06 AM

Ugonjwa wa Ebola umeingia nchini kufuatia watu wawili wanaodhaniwa kuwa na maambukizi yake kuwasili nchini.
 
‘Wagonjwa’ hao wamepelekwa katika kituo maalum kilichotengenezwa na serikali kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa huo kilichopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
Mpekuzi jana ilishuhudia watu wawili wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa huo wakiwa wamefikishwa katika kituo hicho maalum, mmoja akitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 
Mmojawapo anayedaiwa kuwa ni raia wa Benin, kabla ya kufikishwa kwenye kituo hicho alipitia katika Hospitali ya AMI iliyopo jijini Dar es Salaam.
 
Wakati mgonjwa wa Benin akifikishwa kituoni hapo, mwingine alifikishwa kituoni hapo huku akitokwa na damu puani zilizokuwa  zimezibwa kwa pamba.
ebola
 
Mwandishi alizungumza na Kaimu Mganga Mkuu wa Dar es Salaam, Dk. Grace Maghembe, ambaye alisema alikuwa ‘bize’ kuwashughulikia hao wagonjwa na kuomba apigiwe simu baada ya saa moja.
 
“Nipo kuna kitu nafanya. Hebu nipigie baada ya saa moja kwa maana nashughulikia wagonjwa hao hao,” alisema na kukata simu huku akionekana kutingwa na jambo kubwa.

Baada ya saa moja Mwandishi alizungumza na Dk. Maghembe ambaye alithibitisha kuwapo kwa wagonjwa wawili, mmoja raia wa Benin na mwingine Mtanzania.
 
Mwandishi pia lilishuhudia harakati za kuandaa eneo la kupokea wagonjwa wa ugonjwa huo eneo la Temeke ambako hadi sasa ni watu hao wawili wanaohofiwa kuwa wagonjwa wa kwanza kutambuliwa nchini.
 
Wakati Tanzania ikivamiwa na janga hilo, Shirika la Afya Duniani (WHO) jana lilitahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo kutokana na kasi ya kuenea kwake Barani Afrika.
 
Hofu hiyo inaelezwa kutokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati huku wasafiri wengi wanaokwenda na kurudi kutoka nchi za Afrika Magharibi wakipitia jijini Nairobi.
 
Taarifa hiyo iliyokaririwa na Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC), WHO imetoa onyo hilo ili nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zijipange kukabiliana na hati ya mlipuko wa Ebola.
 
Hali hiyo inatokea wakati wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wameripotiwa kufa kutokana na ugonjwa huo.
 
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
 
Mgonjwa wa kwanza  wa Ebola, aliripotiwa nchini Guinea Februari mwaka huu kabla ya kuenea hadi Sierra Leone na Liberia.
 
Nigeria imekuwa mwathirika mkubwa wa ugonjwa huo hasa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na misongamano mingi ya watu na inakadiriwa kuwa takribani theluthi moja ya vifo vya Ebola vimetokea nchini humo.
 
EBOLA NI UGONJWA GANI?
Ugonjwa wa Ebola unaenea kwa kasi kwa kuambukizwa na kirusi kinachopatikana katika ukanda wa nchi za joto.
 
Dalili za ugonjwa huo ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa na vidonda kooni.
 
Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanyakazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutoka damu ndani na nje ya mwili.

Taarifa MPYA ya Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebola kuingia Tanzania.

By on 9:06 AM

Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
 
 Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
 
Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.
ebola
 
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

Katibu Mkuu Dk. Slaa atoa pole Msikiti wa Mtambani, ajionea athari

By on 9:00 AM

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Slaa amefika Msikiti wa Mtambani kutoa pole kwa waumini na viongozi wa msikiti kwa niaba ya chama kutokana na tukio la moto lililotokea juzi jioni.

Katibu Mkuu ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani, Prof. Abdalah Safari mbali ya kutoa pole pia alipata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali kujionea madhara ya ya moto huo ambao hadi sasa kwa mujibu wa Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam unakadiriwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zenye thamani ya Tshs. Mil. 600.

Baada ya kuambiwa na Shehe Katimba mahitaji ya dharura kwa wakati huu, Dk. Slaa aliguswa na suala la wanafunzi wa Seminari ya Mvumoni kukosa vitu muhimu kwa ajili ya masomo yao hasa walioko Kidato cha Nne ambao wanajiandaa na mitihani yao ya kuhitimu, ambapo aliomba apewe tathmini ya mahitaji kwa wanafunzi hao ili chama kiweze kushirikiana na shule na wadau wengine kuwasaidia waendelee na masomo!
Katibu Mkuu akiwasikiliza wenyeji Shehe Rajab Katimba, Mkuu wa Seminari na Mvumoni, Maalim wa Msikiti wa Mtambani na Katibu wa Msikiti alipofika kutoa pole na kujionea athari!

Thursday, August 14, 2014

WEMA Atangangaza Dau La Milioni Atakayemuona Mbwa wake

By on 9:45 PM

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake aitwae Vanila aliyepotea hivi karibuni.
Wema Sepetu โ€˜Madamโ€™.
Wema Sepetu ‘Madam’.
Akielezea ishu hiyo, Wema alisema mbwa huyo alikuwa na mwenzake akiishi nao nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo juzikati alikorofishana na mwenzake aitwae Thiona na kuamua kutokomea kusikojulikana.
Mbwa wa Wema Sepetu aitwae Vanila.
Mbwa wa Wema Sepetu aitwae Vanila.
Msanii huyo alisema anaomba yeyote atakayemuona Vanila wake awasiliane naye au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye na atakabidhiwa pesa zake taslimu.

Thursday, August 7, 2014

Msichana wa kihindi aachana na familia yake tajiri na kuhamia kijijini kwa kijana Mkenya

By on 8:24 PM

Tumezoea kuona kwenye filamu au tamthilia simulizi la msichana mrembo anaotoka katika familia ya kitajiri aliyechagua kuyaacha maisha ya raha na kuishi uswahili na kijana anaempenda.
Huko Kenya, kumeripotiwa tukio halisi lililovuta hisia za wengi na kuzungumzwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, ambapo msichana wa kihindi ameamua kuachana na familia yake tajiri na kuambatana na kijana wa Kenya aliyezama nae kwenye vilindi vya mahaba.
Msichana huyo wa kihidi anaifahamika kwa jina la Sarika Patel, ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu, Timothy Khamala uamuzi ambao ni nadra kutokana na mila na desturi za kihindi na kilichoshangaza zaidi ni kuwa wawili hao wanaishi maisha duni kijijini.
 Kwa Sarika, maisha ya umasikini sio kikwazo cha kulipata penzi la kijana Timothy aliyenasa kwenye penzi lake.
Safari ya penzi la Sarika na Timothy ilianzia nyumbani kwao Sarika ambapo kijana Timothy alikuwa akifanya kazi na baadae kutimuliwa kwa kudhaniwa kuwa ana uhusiano na princess wa jengo hilo (Sirika) jambo ambalo lilikuwa kweli.
Ingawa wawili hao wamejitoa na kuendelea kuishi pamoja licha kukiri kuwa wanakabiriwa na changamoto kubwa ya kutengwa na jamii ya upande wa familia ya kwao Sarika kwa kuwa kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwa mujibu wa mila na desturi zao, ambapo watu wa jamii sawa ndio wanaooana.
Hata hivyo, Sarika ameelezea msimamo wake kuwa utofauti wa rangi na tamaduni au ufukara wake hauwezi kumtenga na mpenzi wake wa dhati Timothy.
Mapenzi sio pesa, mapenzi ni moyo.

Friday, July 11, 2014

WAZIRI WA MAZINGIRA AKANUSHA KUTUMIA FACEBOOK YENYE JINA LAKE‏

By on 1:26 AM

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira, Dkt Binilith Mahenge.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo.
Waziri Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani hapo na kusema kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo vibaya kwa kufungua akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi kujiunga na facebook na hana mpango huo. 
Amesema kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu wanaoziamini taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo wakidhani zimetolewa na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si yeye.
 "Ukiangalia pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni uongo mtupu, kwa mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia ya kweli, hii inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri Mahenge.
 Aidha ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia jamii huku akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha kuwapotosha watu kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na atakayebainika sheria iko wazi dhidi yake. 
Hivi karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahadaa watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi
Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete
                              <<BOYA HAPA ULIKE PAGE KWA HABARI ZAIDI>>

DEREVA: SITOI RUSHWA LABDA UNIUE

By on 12:53 AM

Stori:  Issa Mnally
SEKESEKE la aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up na trafiki ambao majina yao hayakujulikana mara moja liliibuka na kuzua maswali mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa yakitajwatajwa.
Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up.
Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka juzi Jumatano, Bamaga, Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.
Katika tukio hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa wakikunjana, ambapo dereva alikuwa akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi) wakati askari huyo wa usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja sheria.
Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo. 
ILIKUWAJE?
Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kikiwa katika pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha maadili hayavunjwi ndipo kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.
Trafiki alisikika akimwambia dereva kuwa amevunja sheria za barabarani huku gari lake likiwa bovu hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi kituoni kwa ajili ya ukaguzi lakini dereva huyo alikataa.
...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake kukamatwa.
DEREVA
Pamoja na kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na mahali alipoegesha hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: “Nawajua nyie trafiki, kazi yenu ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda mniue.“Siendi popote, mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi nimesema silitoi.”
...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa usalama wa barabarani 'trafiki' .
TRAFIKI
Trafiki huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa na makuu, zaidi alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo wake baada ya ukaguzi.
Mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.
Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
“Sasa kama gari lake anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa anajiamini kuwa aliegesha sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli anajua yupo sawa, anatakiwa kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe.
“Wakati mwingine unaweza kuwalaumu tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila shuruti. Sasa anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari atamwachia?
Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
“Anasema eti hatoi kitu, kwani kaombwa rushwa pale au anadhani kila trafiki anayemkamata dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?” alisikika shuhuda mmoja akihoji kwa jazba.
Hata hivyo, pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake lilifanikiwa kuvutwa kuelekea polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine kulifuata.

Watandikwa viboko Pemba kwa kwenda sivyo katika Mwezi Mtukufu

By on 12:52 AM




Vijana wakipata joto ya jiwe baada ya kukutwa mchana wa Ramadhaan Machomanne, Chake Pemba wakifanya mambo kinyume na maadili ya mwezi mtukufu. Picha kwa hisani ya Abdi Suleiman, Pemba

Thursday, July 10, 2014

MAUAJI YA WANAWAKE NACHINGWEA YAENDELEA

By on 11:36 PM

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa miaka, 32 umeokotwa leo na kufanya idadi ya wanawake waliouawa mpaka sasa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kufikia nane.
Wanawake hao nane waliouawa kikatili mpaka sasa wana umri kati ya miaka 18-32.
Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.
Katika kuonyesha kuwa wamekerwa na vitendo hivyo, baadhi ya wananchi wilayani humo, leo wamezingira Kituo Kikuu cha Polisi Nachingwea, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne wakitaka polisi kuwaruhusu kuwawaue watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, amesema wananchi hao wenye hasira walikuwa wamezunguka kituo hicho cha polisi wakitaka kuwaua watuhumiwa watatu wanaoshukiwa kuwa ndio wahusika wa baadhi ya mauaji ya wanawake hao.
(VIDEO:)

ALIYEMNG’ATA HAUSIGELI NA KUMCHOMA PASI AACHIWA KWA DHAMANA

By on 8:46 PM

Amina Said Maige (mwenye miwani) akisubiria kupandishwa kizimbani.Amina akiwa chini ya ulinzi akisubiri kupanda kizimbani....akijiziba kwa aibu kabla ya kupanda kizimbani.Wanaharakati wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakifuatilia kesi hiyo.Wanaharakati wakisubiri kwa hamu kusomwa kwa kesi ya Amina dhidi ya hausigeli wake, Yusta.
YULE mwanamke anayejulikana kwa jina la Amina Said Maige ambaye anakesi ya kumng’ata na kumchoma kwa pasi hausigeli wake, Yusta  Kashinda (20), ameachiwa kwa dhamana.
Amina alisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi, Yohana Yongolo.
Mahakama imemuachi kwa dhamana baada ya masharti yake ya kuwapata waajiriwa wawili pamoja na kiasi cha shilingi milioni tatu kila mmoja kukamilika.
Amina alikamatwa Juni 4 mwaka huu na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa kupatikana na kosa la Kumng’ata, kumchoma kwa pasi na kumpiga mwili mzima, Yusta. Kesi yake ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar ambapo mara ya kwanza alisomewa mashtaka Juni 12 na kesi kuhairishwa mpaka Juni 26 pamoja na Julai 10.
Kesi yake itasomwa tena Julai 22 mwaka huu.
(PICHA / HABARI: DEOGRATIUS MONGELA / GPL)