Polisi
mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha
gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike,
Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya mkoani Morogoro.
Katika
tukio ambalo mwandishi wa habari hizi alilishuhudia, mara tu baada ya
kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na mihogo,
askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake lililokuwa
bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.
Wananchi
waliojawa na hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari hilo na
kutaka kulichoma moto, lakini busara za baadhi yao ziliwezesha kitendo
hicho kutofanyika na baadaye trafiki alifika kudili na tatizo hilo
Mmoja
wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina ya Toyota Baloon
lenye namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto aliyegongwa alikuwa
akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu kichwani.
Mtu
huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti huyo
alikuwa ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi wa
pembeni gari hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha
pikipiki.
Hata
hivyo, siku moja baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza na
baba mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu
aliyemgonga alikwenda hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa
amefariki.
0 comments:
Post a Comment