Ugonjwa
wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na
kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa
vya habari na kuihusisha Tanzania.
Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
Waziri
Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya
kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa
ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili
waliohisiwa.
Kupitia
ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu
vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia
huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje
huutumia.
0 comments:
Post a Comment