Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Sunday, August 17, 2014

Alikiba: Nawaomba watu Wasinikosanishe na Diamond, Sina Ugomvi Naye

By on 6:12 AM

Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.
alikiba

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.
Diamond Platinumz
Diamond Platinumz

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

Thursday, July 10, 2014

Godzilla: Wasanii wengi wa bongo Flava ni waongo, wanadanganya gharama za video na nyumba walizojenga...

By on 4:26 AM

Rapper wa Salasala, Godzilla amewachana baadhi ya wasanii ambao amesema hudanganya jamii kuwa na maendeleo makubwa yanayotokana na kazi ya muziki kwa kutaja gharama kubwa za video na nyumba wanazojenga.
Godzilla amefunguka wakati akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm Jumamosi iliyopita na kuwataka wasanii hao kuacha kudanganya kwa kuwa anafahamu kipato wanachopata wasanii wengi wa Tanzania ukimuweka kando Diamond hakiachani sana.
“Uongo ukiwa mwingi unaharibu sanaa nzima. Mtu anasema ‘sasa hivi nimepiga milioni 50’ kesho unaona anafanya kazi na Adam Juma huyu huyu, hajaenda hata huko wapi.
“Wasanii wengi wa Bongo Flava wengi sana wamekaa kiungo uongo, wanaongeza digit. Unajua mbongo akikwambia kitu sasa hivi unadivide by two. It’s a lie man. Wote tunafanya shows zilezile, pengine hata wasanii wa hip hop wanafanya shows nyingi hata zaidi ya wasanii wa bongo flava.
“Tumchukulie mtu fulani (wa bongo flava) umuweke hata na Joh Makini pale nani anafanya shows nyingi. Joh yuko kwenye mizunguko kila siku. Pengine hata hao akina Fid Q wanapata hela nyingi zaidi. Kuongeza digit na kujizoom..hiyo ndio, na watu wa media mnavyoichukua the whole picture hapo ndio mambo mnayapoteza.”
Godzilla amegusa pia kuhusu gharama za nyumba zinazotajwa na baadhi ya wasanii kuwa zimetokana na matunda ya kazi ya sanaa kuwa sio za kweli.
“Huyu kajenga nyumba ya milioni 150, kwa muziki gani? Endorsement zote tunaziona na tunasikia kabisa amepata bei gani kutoka kwenye ile deal. Watu wanaadd digit na watu wanakubali. Wanaonekana wao kweli wanafanya kazi na wengine hawako serious, it’s a lie.”
Rapper huyo wamewataka wasanii wenzake kuwa wakweli kwa kuwa hauwezi kuwa mkubwa kwa kudanganya na kupost kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusu matunda ya maendeleo yako.
“The Only artist amepata hela zake amemake amekuwa successful ameenda mbali ni Diamond peke yake. Na kila mtu anaona kaenda hapa kapiga hapa, wengine wana-double.”
Ameitaka Media kuzifuatilia taarifa za wasanii wa Bongo Fleva kabla ya kuzifanya kuwa habari kubwa na kuwashusha wasanii wa hip hop kuonekana wao hawafanyi video zenye kiwango kikubwa kutokana na kutopata kipato kama wale waimbaji.
Amesema kitu ambacho kitasaidia zaidi muziki wa Tanzania ni kuwa wakweli ili wadau na serikali ione picha halisi ya kinachoendelea kwenye muziki ili kuweza kusaidia kuuinua. Na kwamba njia pekee ni ile aliyoipendekeza rais Kikwete kuwa Makampuni yawaamini wasanii na kufanya nao kazi
                           <<LIKE PAGE HAPA KWA HABARI KILA SIKU>>

Tuesday, July 8, 2014

AIBU: BRAZIL YAPIGWA 7-1 NA UJERUMANI

By on 8:34 PM

André Horst Schürrle (katikati) akifurahia na wachezaji wenzake wa Ujerumani baada ya kufunga bao la saba dhidi ya Brazil.
 André Schürrle akifunga bao la saba dakika ya 79.
Sammy Khedira akiifungia Ujerumani bao la tano katika dakika ya 29 ya mchezo.
Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Toni Kroos (kulia) baada ya kufunga bao la tatu dhidi ya Brazil usiku huu.
Miroslav Klose (kushoto) akifunga bao la pili kwa Ujerumani na kuvunja rekodi ya kufunga mabao katika michuano ya kombe la dunia akiwa na mabao 16 sasa.
Thomas Muller akifungua milango kwa Wajerumani baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 11.
Muller akishangilia bao lake.
Bao la kufutia machozi la Brazil likiwekwa kimiani na Oscar dakika ya 90.
Wachezaji wa Brazil, Fernandinho, Maicon na David Luiz wakiwa hawaamini kilichotokea katika mechi hiyo. Hapa ni baada ya kupigwa bao la tano.
Fernandinho akihuzunika baada ya Brazil kupigwa bao la tano.
Vilio kwa mashabiki wa Brazil.
Kocha Mkuu wa Brazil, Luiz Felipe Scolari akiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Ujerumani.
Kikosi cha timu ya Ujerumani.
Kikosi cha Brazil kilichokwaana na Ujerumani bila ya Neymar.
MWENYEJI wa michuano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil, ameyaaga mashindano hayo kwa aibu baada ya kupokea kipigo hevi cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani.
Brazil imeondolewa katika michuano hiyo hatua ya nusu fainali na italazimika kucheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na timu itakayopoteza mechi ya leo kati ya Uholanzi na Argentina.
Mabao ya Ujerumani ambao wamelichukua kombe hilo mara tatu yamewekwa kimiani na: Muller, 11, Klose, 23, Kroos, 24, 26, Khedira, 29, Schurrle, 69, 79 huku bao la kufutia machozi la Brazil likifungwa na Oscar, 90.
Kwa matokeo ya leo, Ujerumani wanasubiri kucheza fainali na mshindi wa mchezo wa baadaye kati ya Uholanzi na Argentina.

NIKAPATA SHILINGI ELFU TATU HII KAZI NILIANZA KUIFANYA SAA NNE ASUBUHI MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI. "

By on 6:04 AM

KALA JEREMIAH AMPONZA RAPPER GAZUKO ASHAMBULIWE NA MASHABIKI


Katika hali isiyo ya kawaida ila imemtokea Rapper anayefanya vizuri katika anga la gospel hip hop huyu si mwengine bali ni Gazuko ambaye sasa hivi anafanya vizuri na video yake ya Acha kulia.
siku kadhaa zilizopita Gazuko alipiga picha akiwa kwenye kifusi cha mchanga na kupost mtandaoni kupitia account yake ya facebook Gazuko Junior nakuandika ujumbe huu
"MPANGO WA LEO MCHANA ULIKUWA HIVI BAADA YA KUAMKA BILA KUWA HATA NA SHILINGI MIA IKANIBIDI NIINGIE MTAANI KUTAFUTA KAZI ILI SIKU IENDE NAMSHUKURU MUNGU NILIPATA KAZI HII
Ambapo ujumbe huo ulipelekea maon mbali mbali kutoka kwa mashabiki wa Gazuko na wengine kumwambia kuwa jamaa amefulia kwa maana game limemuacha lakin Gazuko amekanusha kwa kusema kuwa hiyo picha aliyoiweka ni kama kiashiria cha wimbo wake mpya utakaofuata baada ya kazi yake ya acha kulia hivyo hiyo style ya kutanguliza hiyo picha ameicopy kutoka kwa Kala Jeremiah.
picha hii ndio aliyoiiga Gazuko na kuamua kupiga yake akiwa anasomba mchanga na kupost mtandaoni na mwisho wa siku ikamletea dharau..hii ni picha ya Kala Jeremiah akiwa na msanii Ney wa mitego ilisambaa kabla ya kuachiwa kwa wimbo wa simu ya mwisho wa Kala.