Thursday, July 10, 2014

Godzilla: Wasanii wengi wa bongo Flava ni waongo, wanadanganya gharama za video na nyumba walizojenga...

By on 4:26 AM

Rapper wa Salasala, Godzilla amewachana baadhi ya wasanii ambao amesema hudanganya jamii kuwa na maendeleo makubwa yanayotokana na kazi ya muziki kwa kutaja gharama kubwa za video na nyumba wanazojenga.
Godzilla amefunguka wakati akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm Jumamosi iliyopita na kuwataka wasanii hao kuacha kudanganya kwa kuwa anafahamu kipato wanachopata wasanii wengi wa Tanzania ukimuweka kando Diamond hakiachani sana.
“Uongo ukiwa mwingi unaharibu sanaa nzima. Mtu anasema ‘sasa hivi nimepiga milioni 50’ kesho unaona anafanya kazi na Adam Juma huyu huyu, hajaenda hata huko wapi.
“Wasanii wengi wa Bongo Flava wengi sana wamekaa kiungo uongo, wanaongeza digit. Unajua mbongo akikwambia kitu sasa hivi unadivide by two. It’s a lie man. Wote tunafanya shows zilezile, pengine hata wasanii wa hip hop wanafanya shows nyingi hata zaidi ya wasanii wa bongo flava.
“Tumchukulie mtu fulani (wa bongo flava) umuweke hata na Joh Makini pale nani anafanya shows nyingi. Joh yuko kwenye mizunguko kila siku. Pengine hata hao akina Fid Q wanapata hela nyingi zaidi. Kuongeza digit na kujizoom..hiyo ndio, na watu wa media mnavyoichukua the whole picture hapo ndio mambo mnayapoteza.”
Godzilla amegusa pia kuhusu gharama za nyumba zinazotajwa na baadhi ya wasanii kuwa zimetokana na matunda ya kazi ya sanaa kuwa sio za kweli.
“Huyu kajenga nyumba ya milioni 150, kwa muziki gani? Endorsement zote tunaziona na tunasikia kabisa amepata bei gani kutoka kwenye ile deal. Watu wanaadd digit na watu wanakubali. Wanaonekana wao kweli wanafanya kazi na wengine hawako serious, it’s a lie.”
Rapper huyo wamewataka wasanii wenzake kuwa wakweli kwa kuwa hauwezi kuwa mkubwa kwa kudanganya na kupost kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusu matunda ya maendeleo yako.
“The Only artist amepata hela zake amemake amekuwa successful ameenda mbali ni Diamond peke yake. Na kila mtu anaona kaenda hapa kapiga hapa, wengine wana-double.”
Ameitaka Media kuzifuatilia taarifa za wasanii wa Bongo Fleva kabla ya kuzifanya kuwa habari kubwa na kuwashusha wasanii wa hip hop kuonekana wao hawafanyi video zenye kiwango kikubwa kutokana na kutopata kipato kama wale waimbaji.
Amesema kitu ambacho kitasaidia zaidi muziki wa Tanzania ni kuwa wakweli ili wadau na serikali ione picha halisi ya kinachoendelea kwenye muziki ili kuweza kusaidia kuuinua. Na kwamba njia pekee ni ile aliyoipendekeza rais Kikwete kuwa Makampuni yawaamini wasanii na kufanya nao kazi
                           <<LIKE PAGE HAPA KWA HABARI KILA SIKU>>

0 comments:

Post a Comment