Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea na ziara ya kikazi Jijini
Mwanza ambapo leo amezindua kivuko cha MV.TEMESA kitakachofanya safari
zake kutokea Luchele kupitia mwambao wa ziwa Victoria.
Kivuko hiki
kimetengenezwa/kimejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 640 na ni
kivuko pekee chenye mwedo kasi kuliko vyote Tanzania, kina uwezo wa
kubeba tani 65.
Wengine
walioshiriki katika uzinduzi huo ni Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi), Mhandisi Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza),
Mkuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Bodi zilizo chinin ya Wizara ya Ujenzi,
Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa TEMESA, wafanyakazi wa
SUMATRA pamoja na wananchi.
Aidha,
Dkt.Magufuli amesafiri mpaka Singida na kuelekea kwenye ujenzi daraja la
Mbutu linalojengwa na Wakandarasi Wazalendo - Mbutu JV kwa gharama ya
shilingi bilioni 12.
Kwa ujumla
kazi za ujenzi wa daraja zimefikia asilimia 95 ambapo deki la daraja
limekamilika. Ukubwa wa daraja hilo umechukua takribani urefu wa
kilomita tatu. Katika ukaguzi huo, Waziri wa Ujenzi aliambatana na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya, Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Wenyeviti wa Bodi na Wananachi.
0 comments:
Post a Comment