Jitihada za ujenzi wa barabara ya Ludewa Lupingu zikiendelea.
Serikali Imesema Itawafuta Kazi Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi ya Ujenzi Chini ya Kiwango
Huku Ikiwaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS
Kuwasilisha Majina ya Wakandarasi Wazembe Ili Hatua za Kisheria
Zichukuliwa Dhidi Yao.
Kauli Hiyo Imetolewa na Naibu Waziri wa
Ujenzi Gerson Lwenge Kwenye Kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa
Njombe Baada ya Wajumbe wa Kikao Hicho Kumlalamikia Mkandarasi wa
Kampuni ya Nandra Kuendelea Kujenga Barabara za Lami Chini ya Kiwango
Mkoani Hapa.
Naibu Waziri Huyo wa Ujenzi Amewataka Mameneja wa Wakala wa Barabara Kote Nchini Kusimamia Kwa Karibu Miradi ya Barabara Inayoendelea Kujengwa na Kubaini Wakandarasi Wanaofanya Kazi Chini ya Kiwango Ili Serikali Ifutwa Katika Orodha ya Makandarasi Nchini.
Akizungumzia Kuhusu Ujenzi wa Daraja Katika Mto Ruhuhu Linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma Naibu Waziri Lwenge Amesema Daraja Hilo Linatarajiwa Kujengwa Hivi Karibuni na Kurahisisha Miundombinu ya Mawailiano Baina ya Wananchi wa Maeneo Hayo
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kikao Hicho Keptein Mstaafu Aseri Msangi Ambaye Pia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ameagiza Kuitwa Mkandarasi Huyo Anayelalamikiwa wa Kampuni ya Nandra Ili Kueleza Sababu za Kuendelea Kufanya Kazi Chini ya Kiwango Licha ya Kuendelea Kupewa Kazi Huku Akiutahadharisha Uongozi wa TANROADS Mkoa Kuwajibika Juu ya Suala Hilo.
Awali Baadhi ya Wajumbe wa Kikao Hicho Wakiongozwa na Mbunge wa Makete Dkt. Binelithi Mahenge Wamesema ni Vema Serikali Mkoani Njombe na Wakala wa Barabara Mkoa Kuwa Makini na Mkandarasi Huyo Kutokana na Kushindwa Kutekeleza Miradi ya Ujenzi Kwa Wakati na Kiwango Kinachotakiwa Huku Akitolea Mfano Barabara Wilayani Makete Yenye Urefu wa Kilomita 1.5 Ambayo Ametekeleza Kwa Asilimia 10 Tu.

Na Gabriel Kilamlya
0 comments:
Post a Comment