Friday, July 4, 2014

MASTAA WAPONDWA KWA KUFUTURISHA KWA NINI SOMA HAPA......

By on 6:18 AM

Stori: Mwandishi Wetu
VIONGOZI kadhaa wa dini ya Kiislamu jijini Dar, wamewaponda baadhi ya watu maarufu wanaotumia fedha nyingi kuwafuturisha watu kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakisema jambo hilo ni sawa na unafiki na kujionyesha.
Aunt Ezekiel (aliyesimama mbele) akihudumia futari wakati wa mfungo wa Ramadhani mwaka jana.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamesema kufuturisha ni jambo zuri, ila baadhi ya mastaa wamekuwa wakifanya hivyo kwa kujionyesha.
“Mimi sipingi wao kufanya hivyo ila wafuate taratibu, huwezi kuwafuturisha watu ambao hawajafunga na wengine wakitoka hapo wanakwenda kumuasi Mungu.
“Wapo ambao wanafuturu kisha wakitoka hapo wanakwenda kushushia na bia, kuwafuturisha watu wa sampuli hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu,” alisema Ustadhi Yahaya wa Kinondoni jijini Dar.
Naye Shehe Issa Salim wa msikiti mmoja uliopo Buguruni jijini Dar alisema: “Usahihi wa kufuturisha ni kufanya hivyo kwa wale wanaohitaji tena bila kujionesha, kuna watoto yatima, kwa nini wasiende huko?
Msanii wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho (kushoto), akikandamiza futari na mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima mwaka jana.
“Ninachoweza kusema ni kwamba, kama hawatafuata misingi, watajikuta badala ya kufuturisha, wanawalisha watu chakula cha jioni.”
Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa kufuturisha watu wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu kuonyesha mshikamamo miongoni mwa waislamu.
source:GP                              

<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>> 

0 comments:

Post a Comment