Tuesday, July 8, 2014

AIBU: BRAZIL YAPIGWA 7-1 NA UJERUMANI

By on 8:34 PM

André Horst Schürrle (katikati) akifurahia na wachezaji wenzake wa Ujerumani baada ya kufunga bao la saba dhidi ya Brazil.
 André Schürrle akifunga bao la saba dakika ya 79.
Sammy Khedira akiifungia Ujerumani bao la tano katika dakika ya 29 ya mchezo.
Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Toni Kroos (kulia) baada ya kufunga bao la tatu dhidi ya Brazil usiku huu.
Miroslav Klose (kushoto) akifunga bao la pili kwa Ujerumani na kuvunja rekodi ya kufunga mabao katika michuano ya kombe la dunia akiwa na mabao 16 sasa.
Thomas Muller akifungua milango kwa Wajerumani baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 11.
Muller akishangilia bao lake.
Bao la kufutia machozi la Brazil likiwekwa kimiani na Oscar dakika ya 90.
Wachezaji wa Brazil, Fernandinho, Maicon na David Luiz wakiwa hawaamini kilichotokea katika mechi hiyo. Hapa ni baada ya kupigwa bao la tano.
Fernandinho akihuzunika baada ya Brazil kupigwa bao la tano.
Vilio kwa mashabiki wa Brazil.
Kocha Mkuu wa Brazil, Luiz Felipe Scolari akiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Ujerumani.
Kikosi cha timu ya Ujerumani.
Kikosi cha Brazil kilichokwaana na Ujerumani bila ya Neymar.
MWENYEJI wa michuano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil, ameyaaga mashindano hayo kwa aibu baada ya kupokea kipigo hevi cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani.
Brazil imeondolewa katika michuano hiyo hatua ya nusu fainali na italazimika kucheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na timu itakayopoteza mechi ya leo kati ya Uholanzi na Argentina.
Mabao ya Ujerumani ambao wamelichukua kombe hilo mara tatu yamewekwa kimiani na: Muller, 11, Klose, 23, Kroos, 24, 26, Khedira, 29, Schurrle, 69, 79 huku bao la kufutia machozi la Brazil likifungwa na Oscar, 90.
Kwa matokeo ya leo, Ujerumani wanasubiri kucheza fainali na mshindi wa mchezo wa baadaye kati ya Uholanzi na Argentina.

0 comments:

Post a Comment