Wednesday, July 9, 2014

KAMA UNA TABIA HIZI HUWEZI KUFANIKIWA KAMWE MAISHANI MWAKO

By on 2:47 AM


1. KUMSIKILIZA KILA MTU
Kama kila anayekuambia kitu kuhusiana na unachofanya unamsikiliza nakuhakikishia hutopiga hatua kubwa. Katika jambo lolote unalofanya kuna watu watakutia moyo na kuna wengine watakukatisha tamaa. Wapo watakaokwambia haiwezekani au huwezi. Tena wanaokwambia haiwezekani watakupa mpaka mifano ya walioshindwa. Kama unataka kufikia mafanikio makubwa acha kuwasikiliza watu wanaokukatisha tamaa, chagua ni kitu gani unatafanya na anza kukifanyia kazi mpaka ufikie mafanikio yako.
2. UNAFANYA KILE AMBACHO KILA MTU ANAFANYA
Huwezi kuamini ila iko hivi, mafanikio makubwa yanakuja pale ambapo unakwenda hatua ya ziada. Kwenye kila unachofanya kuna hatua ya ziada ambapo kama ukienda hatua hiyo utafikia mafanikioa makubwa sana. Kama unaamka asubuhi, unakwenda kazini, unafanya kazi ulizopangiwa, jioni unarudi nyumbani, unalala na kesho unarudia tena huo mzunguko sahau kuhusu mafanikio makubwa. Kama unafanya biashara kama kila mtu anavyofanya kwa mtindo huo huo na mbinu hizo hizo ambazo kila mtu anayefanya biashara hiyo anatumia unasogeza siku tu. Kama unataka kufikia mafanikio makubwa NENDA HATUA YA ZIADA. Kama unaishi maisha ya bwana mike utasubiri sana na hutofikia mafanikio makubwa.
3. UNATUMIA MUDA HOVYO
Poteza milioni mia moja, unaweza kuzitengeneza tena baada ya muda fulani, poteza sekunde moja ndio umeisahau kabisa. Hakuna kitu chenye thamani zaidi ya muda, lakini ndio tunautumia kizembe kuliko kitu chochote kile. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa lazima uweze kuwa na matumizi mazuri ya muda wako. Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi, kuna vyombo vya habari, simu, email, mitandao ya kijamii na maongezi mengine yanayokusubiri wewe kila siku. Usipokuwa makini unaweza kuona unakwenda na wakati kumbe unakwenda nje ya mstari wa mafanikio.
kitabu kava tangazo
4. UNAPENDA MAJIBU YA HARAKA
Sijui ni kitu gani kimeharibu dunia kwa sasa ila kizazi cha sasa kinapendelea majibu ya haraka kuliko vizazi vivlivyopita. Unataka uanze biashara leo na mwezi ujao uwe umetengeneza faida mara mbili ya mtaji!! Yaani unataka upande mchungwa leo na wiki ijayo uanze kula machungwa. Hakuna kitu kama hicho ndugu yangu, mambo mazuri yanahitaji subira na yanahitaji uvumilivu. Usidanganyike na kelele unazopigiwa na watu kwamba fanya hivi utafikia mafanikio ya haraka, hayo ni matangazo ili kufaidisha biashara zao. Huwa napenda kutumia mfano huu mara kwa mara, huwezi kuwachukua wanawake tisa ukawabebesha ujauzito mmoja ndani mwezi mmoja wakatoa mtoto, kama unatafuta njia ya mkato ya kufikia mafanikio unaweza kuyapata ila hutofika mbali.
5. UNA MATUMIZI MABOVU YA FEDHA ZAKO
Hili nalo linatabia ya kushangaza sana. Ukiangalia kwa makini, waliofanikiwa kifedha wana matumizi tofauti kabisa na wale wanaolalamika kutokuwa na fedha kila siku. Wakati wale wenye fedha nyingi wakitafuta sehemu za uwekezaji, wale wanaozipata kidogo wanatafuta viwanja vya kuzitumbua. Hata kama unapata fedha kidogo kiasi gani ni lazima uwe na kiwango ambacho uaweka pembeni. Jilipe wewe kwanza kwenye kila kipato unachopata na hii itakusaidia kuweza kuwa na maisha yasiyo na hofu juu ya fedha. Kujua zaidi jinsi ya kujilipa wewe kwanza soma makala hii unamlipa kila mtu kasoro huyu mmoja wa muhimu

0 comments:

Post a Comment