Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Saturday, August 16, 2014

NDANI YA HABARI: Watoto 11 chumba kimoja, watumikishwa kuuza vitumbua

By on 12:07 AM
“Hao watoto hatujawaiba, tumewatoa kwao huko mikoani na biashara wanazofanya ni hizo ndogondogo wala siyo ngumu. Wengine hapa hawana baba wala mama wanazunguka tu mitaani. Wameona kuliko kuiba, ni bora waje wafanye kazi ili wapate pesa za kujikimu,” anasema Fatuma. 
Na Elias Msuya, Mwananchi

  • Mmiliki wa biashara hiyo asema alifanya hivyo kuwasaidia kwa kuwa wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.


Pengine takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) kwamba watoto wapatao milioni 250 wanatumikishwa katika ajira mbalimbali duniani kote, zikawa ndogo kulingana na hali halisi kwa kuwa kila kukicha, mapya huibuka.
Ajira hizi zinapaswa kupigwa vita kwa kuwa siyo tu zinawanyima haki za msingi watoto, bali zinachochea umaskini kwa familia na taifa kwa jumla.
Hassan Abdallah mkazi wa Tabata ni mmoja kati ya wanaoshiriki katika biashara hii haramu ya kuajiri watoto. Hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuajiri watoto 11 kwa kazi za kuuza vitumbua huku akiwahifadhi ndani ya chumba kimoja.
Kati ya waajiriwa hao, watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wako wanane.
Katika makazi hayo, watoto walimwonyesha mwandishi wa habari hizi banda la mabati wanalotumia kwa malazi likiwa kando ya nyumba ya mwajiri wao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisukuru, Lukresia Msuya anasema kuwa Abdallah na mkewe Fatuma Shomari wamekuwa wakiwafuata watoto hao mikoani na kuwaleta jijini Dar es Salaam kuwatumikisha kuuza vitumbua mitaani.
“Tulipigiwa simu juzi na katibu wa CCM wa mtaa akisema kuwa kuna jambo la muhimu. Hapo ndipo aliponionyesha nyumba hii ambayo ina watoto wanaotumikishwa kuuza vitumbua. Tukawakusanya na kuwapelekapolisi,” anasema Msuya.
Amewataja watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo kuwa ni pamoja na Furaha Samuel, Steven Tudius, Amani Adison, Yusuf Simon, Richard Zakaria, Kackson Jackson Michael, Elia Wilson, Boniface Lawrence, Baraka Francis, Zamda Yumpunju, Jema Ramadhani na Haji Ramadhani.
Msuya amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kisukuru kisha kuhamishia shauri hilo Stakishari ambako Abdallah aliwekwa ndani.
“Nikiwa kama mzazi inaniuma kuona watoto hawa wadogo wenye umri kati ya 17 na 12 wakifanyishwa kazi kama hizi. Nawaomba wazazi wawakumbatie watoto kama vifaranga vya kuku. Mtoto wa miaka 12 umfanyishe kazi, halafu utamlipa nini kama siyo kumdhulumu?” alihoji.
Jinsi walivyokamatwa
Akieleza jinsi alivyogundua suala hilo, katibu wa CCM wa Mtaa wa Kisukuru, Thomas Matiku anasema kuwa alipewa taarifa na wananchi wakati akitoka Buguruni.

Thursday, July 10, 2014

HABARI KAMILI KUHUSIANA IRENE UWOYA KUKUTANA NA MKENYA KWENYE HOTELINI

By on 4:58 AM


Latest news zinasema kuwa star wa filamu nchini Irene Uwoya amekutana faragha Nairobi, Kenya na star mwenzake wa muziki toka nchini humo Jaguar.
Chanzo kimoja kilicho karibu na Uwoya kikizungumza nasi kimesema kuwa wawili hao kuna deal wanafikiria kufanya pamoja lakini hana uhakika mpaka sasa ni deal gani "Uwoya na Jaguar wamekutana faragha kuna issue zao wana-talk ila sijui ni deal gani hizo, nitakupa updates" kilisema chanzo hicho.


Hata hivyo chanzo kingine kutoka Kenya kimesema kuwa kimewaona Uwoya na Jaguar katika hotel moja jijini Nairobi wakiwa katika mikao ya kimahaba a.k.a zero distance " Hi, I have seen Irene Uwoya with Jaguar in a hotel in Nairobi they looked like an item, hawa celebs sio predicted" kilisema chanzo hicho
Mwandishi alijaribu kumsaka Uwoya lakini namba yake haikupatikana, hata hivyo juzi Uwoya aliweka picha akiwa Julius Nyerere International Airport akisema anaenda Nairobi ingawa hakuweka wazi kama anaenda kikazi au lah .

Saturday, July 5, 2014

LUCY KOMBA ATENGWA BONGO MOVIE... SABABU SOMA HAPA ZAIDI

By on 12:07 AM

Stori: Mayasa Mariwata
STAAwa sinema za Kibongo, Lucy Komba, amedaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie kwa kosa la kuwatolea lugha za kejeli.Staa wa sinema za Kibongo, Lucy Komba,
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Bongo Movie wamemsusia msanii huyo katika vikao vya harusi yake kwa madai kuwa aliwahi kuwaponda kwenye vyombo vya habari kuwa klabu hiyo si chochote kwake.
Alipotafutwa na paparazi wetu, Lucy ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha Septemba, mwaka huu, alisema hakumbuki kama aliwahi kuwakejeli wasanii hao isipokuwa wengi wamekuwa wakimjadili kwa suala hilo na sasa hawahudhurii kwenye vikao vya harusi yake.
“Mimi hata sikumbuki kama niliwahi kuongea hayo kwenye vyombo vya habari na kama niliongea labda walinielewa tofauti na kauli niliyoitoa, sioni sababu ya kuwekeana bifu ila kwa anayetaka acha aendelee,” alisema Lucy.
SOURCE:GP
<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>> 

MADAI YA KUCHEPUKA KAJALA ACHARUKA

By on 12:04 AM

Stori: Musa Mateja
BAADA ya kuzagaa kwa taarifa mbalimbali kwamba mwigizaji wa Bongo, Kajala Masanja anachepuka nje, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli wowote.
Mwigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja
Mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiposti taarifa mbalimbali zinazomhusisha Kajala kutembea na wanaume tofauti kitu ambacho mwenyewe amesema hakina ukweli na wanaosambaza uvumi huo, wakome.
Akizungumza na mwanahabari wetu Julai 3, mwaka huu alisema wanaoeneza habari za yeye anachepuka wanamtafuta ubaya kwani hana mpango wowote wa kuolewa wala kuishi na mwanaume kwa sasa.
“Waniache, mtu akisema nina mwanaume alishawahi kuniona? Sina mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu,” alisema Kajala.
Kwenye mahojiano hayo, Kajala alisisitiza kuwa, haoni sababu ya yeye kuchepuka wakati mumewe Faraja Augustino yupo hai na anaamini ipo siku atatoka gerezani na ataendelea na maisha ya ndoa yake kama ilivyokuwa zamani.
Kajala Masanja akiwa kwenye pozi
“Kiukweli sioni haja ya kuolewa na mwanaume mwingine tena wakati ni wazi ipo siku mume wangu atakuwa huru, naomba ieleweke kwamba sina mpango na mwanaume yeyote na sasa namgonjea atoke tuendelee na maisha yetu,” alisema Kajala.
Mume wa Kajala, Faraja Agustino anatumikia kifungo cha miaka 7 baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi milioni 200 kufuatia kesi ya kutakatisha fedha iliyokuwa ikimkabili.
Kwenye kesi hiyo, Kajala ambaye naye alihusishwa, alilipiwa faini ya shilingi milioni 13 na mwigizaji Wema Sepetu, kifungo cha miaka mitano kikamuepuka.
<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>> 

Friday, July 4, 2014

MAPICHA: EBWANA EH!!! MTAZAME K-LYINN NA WATOTO WAKE KWENYE JUMBA LAKE

By on 11:34 PM




Mwanamama Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyinn leo kupitia ukurasa wake INSTAGRAM amshea nasi picha hizi na video clip akiwa na watoto wake mapacha....!!!!! ITS ALL ABOUT GOOD LIFE MAZEEE!!!!
<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>>

AFARIKI WAKATI AKIZUIA MAITI ISIKANYAGWE NA MAGARI

By on 11:16 PM

WATU wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Ndahani aligongwa 

na gari isiyofahamika kwa kuwa lilikimbia baada ya ajali hiyo.

Alisema Ndahani alikuwa akitaka kuzuia magari yasiukanyage mwili wa Onesmo Yarimunda aliyefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Prince Muro alipokuwa akivuka barabara.

Kamanda Wambura, alisema Yarimunda (36), mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo aina ya Scania, juzi, saa 3 usiku maeneo ya Kibamba.

Maiti zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha. Dereva wa basi la Muro, Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha anashikiliwa na polisi

<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>>

Kuhusu shekh wa Arusha aliyejeruhiwa wakati anakula Daku.

By on 12:47 PM

wakiswali
Kutoka Arusha taarifa ambayo imetangazwa kupitia Leo tena ambayo imetolewa kama breaking news ni kuhusu Sheikh wa msikiti wa Qiblatan Sood Ally Sood (37) uliopo eneo la Kilombero jijini Arusha kulipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku na kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imedaiwa kuwa Sheikh huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili sehemu za mapajani pamoja na Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Mbali na Sheikh huyo pia kuna mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) ambaye ni mkazi wa Dar es salaam naye amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
MAONI


Arusha hali si shwari..... yachafuka tena,Bomu lingine lalipuka.

By on 7:02 AM



Photo 

Kwa habari tulizozipata hivi punde ni kwamba muda mfupi uliopita kumetokea mlipuko wa mabomu katika mitaa ya Ngarenaro nyuma ya soko la Kilombero.
 Chanzo cha mlipuko huo hakijajulikana hadi hivi sasa.
Bomu hilo limesababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo huku majeruhi hadi hivi sasa wako katika hospitali ya Mount Meru.


PhotoPhotoPhoto



Photo

MASTAA WAPONDWA KWA KUFUTURISHA KWA NINI SOMA HAPA......

By on 6:18 AM

Stori: Mwandishi Wetu
VIONGOZI kadhaa wa dini ya Kiislamu jijini Dar, wamewaponda baadhi ya watu maarufu wanaotumia fedha nyingi kuwafuturisha watu kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakisema jambo hilo ni sawa na unafiki na kujionyesha.
Aunt Ezekiel (aliyesimama mbele) akihudumia futari wakati wa mfungo wa Ramadhani mwaka jana.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamesema kufuturisha ni jambo zuri, ila baadhi ya mastaa wamekuwa wakifanya hivyo kwa kujionyesha.
“Mimi sipingi wao kufanya hivyo ila wafuate taratibu, huwezi kuwafuturisha watu ambao hawajafunga na wengine wakitoka hapo wanakwenda kumuasi Mungu.
“Wapo ambao wanafuturu kisha wakitoka hapo wanakwenda kushushia na bia, kuwafuturisha watu wa sampuli hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu,” alisema Ustadhi Yahaya wa Kinondoni jijini Dar.
Naye Shehe Issa Salim wa msikiti mmoja uliopo Buguruni jijini Dar alisema: “Usahihi wa kufuturisha ni kufanya hivyo kwa wale wanaohitaji tena bila kujionesha, kuna watoto yatima, kwa nini wasiende huko?
Msanii wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho (kushoto), akikandamiza futari na mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima mwaka jana.
“Ninachoweza kusema ni kwamba, kama hawatafuata misingi, watajikuta badala ya kufuturisha, wanawalisha watu chakula cha jioni.”
Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa kufuturisha watu wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu kuonyesha mshikamamo miongoni mwa waislamu.
source:GP                              

<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>> 

Mhalifu ‘handsome’ zaidi duniani Jeremy Meeks kupata shavu la modelling la tshs mil50 kwa mwezi

By on 3:39 AM
Jeremy Meeks, aliyepewa jina la mhalifu handsome zaidi duniani, anaweza kulipwa hadi dola 30,000 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 50) kutokana na mikataba ya uanamitindo kutoka kwa makampuni yanayohaha kumuajiri.
10447725_777020855652123_5067320508800351604_n
Meeks, 30, ametokea kuwa kipenzi cha wanawake wengi duniani baada ya polisi kuweka picha (mugshot) yake kwenye ukurasa wa Facebook baada ya kukamatwa na silaha za moto katika mji Stockton, Marekani.
Polisi wamedai kuwa jamaa huyo ni miongoni mwa wahalifu hatari zaidi katika mji wa Stockton lakini mugshot yake ilipata umaarufu kwa kupata likes zaidi ya 40,000. Atapandishwa mahakamani Ijumaa hii. Kampuni moja iitwayo Blaze Modelz imeuambia mtandao wa TMZ kuwa inaweza kumtumia Meeks kutangaza viwalo vya Versace na Armani.

BAADA YA KULEWA CHAKARI NJEMBA ZAMLA TIGO MREMBO HUYU

By on 1:54 AM
Top 10 Trending Images in Nairobi This Morning

Wadada bhana mnazidi kutushangaza sisi waungwana hivi inakuaje unapiga mitungi mpaka kiasi unashindwa kutembea kabisa, ni ofa ndo zinakuchanganya ama nini jaribuni kupiga soft basi maana pombe kali hamziwezi wachie wanaume ,,,, sasa huyu bahati nzuri kakutana na msamalia mwema kamsaidia ... angekuwa si huyo waune bila shaka wangejisevia kiroho safi.. dah kuweni makini dada zetu jamani



BREAKING NEWS: MAREKANI YATOA TAHADHARI JUU YA KUTOKEA TISHIO LA KIGAIDI UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE UGANDA LEO

By on 1:53 AM

TISHIO UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa onyo ukisema kuna "tishio dhahiri ... kutoka kundi lisilojulikana" kushambulia uwanja wa ndege wa Entebbe. 


Onyo hilo limechapishwa kweye tovuti ya ubalozi huo kufuatia tahadhari nyingine iliyotolewa na mamlaka za Marekani siku ya Jumatano ya kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege vya Mashariki ya Kati na Ulaya vyenye ndege za moja kwa moja kwenda na kutoka Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, kuna tishio thabiti kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe leo kati ya saa tatu usiku hadi saa tano- imesema taarifa hiyo.

HUU NDIO UKATILI HUU ULIOFANYWA NA MWANASHERIA MAARUFU NCHINI KWA BINTI HUYU SOMA NA UJIONEE HAPA

By on 1:50 AM


1.  Ndugu Wanahakati.
2.  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wasalaam.
Mtoto MELINA amakumbwa na matatizo makubwa sana. Anahitaji msaada wetu sote kama Watanzania na wapenda haki.
Melina ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na kichwani na bosi wake YASINTA RWECHUNGURA ambaye ni mwanasheria mkubwa nchini anahitaji msaada wako.
SIKU 730 au miaka miwili ya unyama na ukatili uliombatana na vipigo mfululizo, vimempa wakati mgumu katika maisha mtoto wa miaka 15, Melina aliyefika katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012 akitokea  kijijini Ishozi- Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za ndani, yaani ‘hausigeli’.
Katika tukio la hivi karibuni na la kusikitisha, lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwa mwanamke huyo YASINTA RWECHUNGURA, Boko-Magengeni jijini Dar ambako Melina alikuwa akifanyia kazi.
Binti huyo ambaye wakati anafika jijini Dar alikuwa na miaka 12, licha ya umri wake kuwa mdogo alifanya kazi kwa bidii ili mshahara wake uweze kuwasaidia wazazi wake ambao hawajiwezi kimaisha kule kijijini.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, Melina alichukuliwa na bosi wake huyo kwa makubaliano ya mshahara wa shilingi  40,000 kwa mwezi huku shilingi 20,000 zikitumwa nyumbani kwao Kagera kwa wazazi wake.
“Lakini katika hali ya kushangaza, bosi wake alikuwa hampi zile shilingi 20,000 kama makubaliano yao yalivyokuwa akisema kwamba anamtunzia kuepuka matumizi mabaya.
“Ikaelezwa kuwa, akiwa ndani ya kazi, binti huyo alijikuta akipata mateso makubwa kama vile kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kukosa, kufanya kazi vibaya au tofauti na maelekezo,” kilisema chanzo.
Akizungumza kwa uchungu na maumivu makali akiwa hospitalini hapo, Melina anaanza kwa kusema:
“Nimechoka sana ndugu zanguni, nimeteseka sana, nisaidieni nirudi kwetu Kagera. Kosa dogo napigwa na blenda na nyaya za kompyuta. Ndiyo maana sehemu mbalimbali za mwili hadi kichwani nina makovu kama hivi”.



“Mara hii ya mwisho nilipigwa na kwanja la kufyekea ndiyo majeraha haya. Wakati akinitesa bosi wangu alikuwa akiniambia hakuna wa kumtisha. Nisaidieni jamani, miaka miwili ya mateso  mfululizo sasa nataka kurudi kwa wazazi wangu japokuwa hawana uwezo tutaishi hivyohivyo tu. “
Mtoto huyo ana makovu (majeraha yaliyopona) 73 kichwani na mwilini mwake ambayo yote yanadaiwa yalitokana na adhabu ya mashambulizi ya kudhuru mwili ingawa haikubainika kama ni kutoka kwa bosi wake huyo au la!
Mnamo tarehe 11 Juni, mwaka huu (2014), saa 3 usiku, Melina alipelekwa  katika hospitali binafsi iliyopo Mbezi, Dar akiwa na majeraha makubwa kichwani. Aliambatana na wanawake watatu, Mama Betty, Mama Winnie na mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rwechungura (Anasemekana ndiye bosi wake).
Kwa kutotaka kuonekana kama wanahusika na huyo motto, walisema kuwa wao ni majirani wanaoishi karibu na binti huyo na walifika hospitalini hapo kwa lengo la kumsindikiza na kujua nini kinaendelea. Swali kama wao hawaishi nae bali ni majirani, je huyo anayeishi nae alikuwa wapi wakati mtoto anapata maswaibu hayo? Na kwanini hawakutaka kutoa namba zao za simu wapoombwa na daktari?
Daktari aliyekuwa zamu usiku huo inasemekana kuwa alishtushwa na hali ya Melina kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi usoni na kichwani.
Daktari kwa kutaka kujua zaidi kilichotokea ndipo akapasua jipu kwamba alikuwa amepigwa na bosi wake na kwamba hata makovu mengine ni majeraha yaliyopona ambayo yalitokana na kipigo cha mara kwa mara.
Habari zinazidi kudai kuwa, daktari huyo aliendelea kuokoa maisha ya Melina kwa kumshona nyuzi karibu kumi na mbili katika maeneo yaliyopasuka  lakini kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, ilibidi aende kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
“Polisi walikwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida walikuta nyumba haina mtu tena ikiwa wazi kwa usiku huo.
“Inasemekana katika wale wanawake watatu waliompeleka Melina hospitali, mtuhumiwa alikuwepo ila alitoroka baada ya polisi kuonesha nia ya kumkamata.
“Hali ya Melina ilizidi kuwa mbaya. Alfajiri ya Juni 12, mwaka huu ilibidi ahamishiwe kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipokelewa na kupewa matibabu. Hali ikazidi kuwa mbaya, akahamishiwa Muhimbili.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,  Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba, mtuhumiwa alitoroka lakini Jumamosi iliyopita alitiwa mbaroni maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, tayari amefikishwa mahakama ya mkazi kinondoni. Kesi ya jinai namba 226/2014, itatajwa tena tarehe 1 Julai, 2014.
OMBI:
1.    Wanaharakati nyote mnaombwa kuhudhuria siku hiyo ya tarehe 1 Julai, 2014 ili kumtia moyo huyo mtoto nakumfariji. Mtoto anahitaji msaada wa kisheria, ikiwemo na fedha za kujikimu.
2.    Kurudishwa shule na kupata mfadhili wa kulipia masomo
3.    Kumchangie mama mzazi wa huyo MELINA aweze kuja hapa Dar Es Salaam ili akamuguuze mtoto wake, ili mtoto aweze kuwa na amani na utulivu kwani kwa sasa hivi ana wasiwasi mkubwa mno kwa kuwazakuwa Yule mbaya wake atamfuata hospitalini na kuweza kumdhuru
TAARIFA ZA KUSIKITISHA
1.    Mtuhumiwa kwa kushirikiana na ndugu zake wamemrubinu baba mtoto huyo, toka afike Dar es salaam hajawahi kuwasiliana na wajomba wa mtoto Melina ambao ndiyo yaliwasiliana na huyo jamaa kumjulisha aliyotokea huku
2.    Inasemekana kuwa mipango inafanyika kuweza kupoteza ushaidi kwa namna yoyote iwayo. Mtoto ana wasiwasi sana na kila wakati anaomba wajomba zake wamtoe hospitali
3.    Pia inasemekana YASINTA RWECHUNGURA kwa kutumia watu Fulani, na ambao walikwenda hospitali wakajitambulisha kwa baadhi ya madaktari kuwa wanahitaji waelewane nano (kuwaonga) ili wayamalize kimyakimya. Hapa maanake hayaeleweki. Kwa upande wa madaktari waliyoelezwa mambo hayo na ndugu zake huyo YASINTA RWECHUNGURA walikataa jambo la eti kuelewana nao. Maswali wametanda kwenye vichwa vya ndugu zake huyo motto MELINA, kuwa je, 1) usalama wa mtoto huyo utalindwa na uongozi wa hospitali ya Muhimbili? 2) Je, uongozi wa juu wa Muhimbili una taarifa hizo? 3) Je, huyo baba wa motto huyo ambaye ametoka nyumbani kagera bila kumshirikisha mamake motto ana nia njema? Kwani inasemekana mipango ilifanywa na ndugu zake YASINTA RWECHUNGURA yakumfuata huyo bwana huko kijijini na kuongea nae kutaka wayamalize.
4.    Baba mtoto huyo amejificha au amefichwa na wabaya wa mtoto wake, swali je, nae anahusika? 1) Kwanini baada ya kupokea taarifa ya yaliyokea kwa motto wake aliamua kufanya vikao vya siri na ndgu zake YASINTA RWECHUNGURA na kuamua kutomtaarufu mke wake na kuamua kuja huku Dar es salaam kisirisiri?
Wanahakati tunawaomba mfuatilie kwa karibu suala hili na vilevile mlisimamie MELINA awe salama na apate haki stahili yake.
Tazama picha zake akiwa hospitali alikolazwa.
TUNAOMBA MSAADA WENU.

WATIFUANA!......... NANI HAO SHUKA HAPO

By on 1:37 AM

Stori: WAANDISHI WETU
MTIFUANO! Mastaa wawili wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wameendeleza ligi ya bifu lao baada Chuchu kujibu mapigo huku malejendari wengine wawili wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’ wakitifuana.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI, CHUCHU
Kwa muda mrefu Johari na Chuchu walidaiwa kuwa kwenye gogoro kubwa kisa kikisemekana ni penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.
CHUCHU AVUNJA UKIMYA
Safari hii Chuchu ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu, ameibuka na kujibu yale yote anayodai yalikuwa yakisemwa vibaya juu yake, mhusika mkuu akiwa ni Johari.
Moja ya tuhuma aliyodai kupachikwa na Johari ni ile ya kwamba amekuwa akitumia vifaa vya Kampuni ya RJ Productions inayomilikiwa na Ray na Johari.
CHUCHU ADAI KUFUATA PENZI
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi jijini Dar, Chuchu alifunguka kwamba huwa anakwenda RJ kufuata mapenzi na si kampuni kwani ana uwezo wa kuwa na kampuni kwa sababu vifaa anavyo na Ray alimkuta akiwa navyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans akipozi.
JOHARI AITWA OLD FASHION
Chuchu ambaye kwa sasa anaonesha mahaba niue kwa Ray alisema kuwa anamshangaa Johari kusema kuwa anatumia vifaa vya RJ na wengine kusema ni mke mwenzake wakati Johari ni ‘old fashion’ kwani aliachwa na Ray kama wanawake wengine na yeye akaingia.
BOFYA HAPA KUMSIKIA CHUCHU LAIVU
“Mimi ndiyo ‘new fashion’, Johari atabaki kuwa ‘old fashion’ kwa Ray, sipendi kabisa watu waseme eti ni mke mwenzangu, mbona alishaachwa siku nyingi? Ukewenza unaingia vipi hapo jamani?” aliwaka Chuchu.
Chuchu aliendelea kutiririka kuwa kamwe hawezi kutumia vifaa vya RJ kwani vya kwake vinamuwezesha kufungua kampuni yake.
JOHARI ANASEMAJE?
Baada ya Chuchu kuwaka vya kutosha, kama ada ya Magazeti ya Global kutafuta mzani wa habari, Johari alitafutwa na kumwagiwa kile alichosema mwenzake ambapo aliomba aachwe kwanza kwani kwa wakati huo alikuwa kwenye kikao kizito akiomba kumpigia mwandishi baada ya kikao.
Baadaye alipopatikana alisema kwa kifupi; ‘No comment’ huku shosti wake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina lake akieleza kuwa, hali si nzuri kwani kuna msuguano mkali wa chini kwa chini.
Staa mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Ray C.
NINI KIMETOKEA?
Miezi kadhaa Johari na Chuchu walidaiwa kutibuana kisa kikielezwa kuwa ni penzi la Ray ambapo mwigizaji mwenzao, Ruth Suka ‘Mainda’ ambaye naye alikuwa mmoja wa wapenzi wa kaka mkubwa huyo, yeye alikaa pembeni na kumwachia Mungu kisa cha yote kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
RAY C, TID
Wakati nyumba ya jirani Bongo Movies kukiwaka mto huo, kwenye muziki wa Bongo Fleva, Ray C na TID Mnyama wanadaiwa kuingia vitani kwa kisa cha kuchekesha.
TID ambaye ni mmiliki wa Top Band ndiye aliyeanza kumuwakia Ray C kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya mwanadada huyo kumuomba wazungumze.
MADAWA YA KULEVYA YATAJWA
Ilidaiwa kwamba TID ambaye amekuwa akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya ‘unga’ huenda alihisi Ray C alitaka kumletea habari za kumsaidia kuachana nayo kupitia dawa za Methadone.
“Njoo tuzungumze TID, wewe ni Msanii Bora Afrika Mashariki, tafadhali tuzungumze tidmnyama,” aliandika Ray C.
Mmiliki wa Top Band, TID Mnyama katika pozi.
RAY C HAKUFAFANUA
Pamoja na kwamba Ray C hakufafanua kile alichotaka kuzungumza na TID baada ya kuandika maneno hayo na kuweka picha ya TID inayotambulisha Refix ya wimbo wake wa Asha, jamaa alianza kuporomosha matusi akimtaka aachane naye kabisa.
BOFYA HAPA UMSIKIE TID
“(tusi) niache mwenyewe, mimi siyo type yako. Pia sitaki kusikia chochote kutoka kwako. Makosa yako ni ya kwako, nakuomba kaa mbali (tusi) na mimi, kamsaidie boyfriend wako, sijawahi kuvutiwa na wewe, nukta,” aliandika TID kwa hasira.
MATUSU MWANZO-MWISHO
Baada ya hapo ndipo zikaibuka kambi mbili, ya upande wa Ray C ilikuwa ikimtukana TID kutokana na kile alichomjibu Ray C ambaye hakutaja nia ya kutaka kuzungumza na TID.
Kuona hivyo, nayo timu ya mashabiki wa TID ilijitoa kimasomaso na kumshambulia Ray C kwa maneno makali kama hayo aliyoyatumia TID yakipambwa na matusi.
Gazeti hili lilipomtafuta TID, mbali na matusi alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi kama kuna mtu ananitafuta, hawezi kunitafuta kwenye Instagram, sijawahi kuwa na matatizo na Ray C.

Ray na Chuchu katika pozi.
“Kwanza sijamuona, nina kama miaka mitano hivi.
“Hivi Ray C anataka kukutana na mimi? Anataka kuongea na mimi? Mbona hajanitafuta miaka yote, ananitafuta sasa hivi? Mimi sijapenda, mwambieni sitaki kuonana naye.
“Nasema sitaki kuongea naye, sitaki kukutana naye, akaongee na maboyfriend wake ambao anafanya nao vitu vibaya, mimi si wa aina yake, aniache na familia yangu, aniache na mama yangu.”
RAY C AMWAGA CHOZI
Baada ya kushuhudia tafrani hiyo, gazeti hili lilimtafuta Ray C ambaye alionesha kusikitishwa na kile alichokisema TID hasa matusi.
“Niliona nimuombe kuonana naye na wala sikusema nilichotaka kumwambia. Nimesikitishwa na namna TID alivyonielewa vibaya.
“Nimeshamtafuta sana hadi kwao ikashindikana, kuna siku nilikutana naye Mwananyamala hospitalini, alikuwa anaumwa, nikamuomba tuongee lakini ilishindikana.
“Nilikuwa simtafuti kwa ubaya, nilitaka aje ofisini tuzungumze, nilitaka tufanye shoo ya pamoja mimi, yeye na Chidi Benz (Rashid Makwilo). Nilitaka tufanye hivyo ili kukemea matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu ni janga la kitaifa.
“Kweli ameniumiza kwa sababu sikuwa na lengo baya hata kidogo, sijawahi kumkosea TID,” alisema Ray C huku akimwaga machozi hivyo mwanahabari wetu akamuomba anyamaze.
Kwa sasa Ray C anaendesha kampeni ya kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya kupitia taasisi yake ya Ray C Foundation ikiwa na slogani ya Tanzania Bila Madawa ya Kulevya Inawezekana.
KUTOKA KWA MHARIRI
Hivi karibuni waigizaji Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja walimaliza tofauti zao hivyo ni vyema wasanii hao nao wakamaliza bifu zao.
CREDIT:GP

EXCLUSIVE: HAYA NDIYO MAJIBU YA ADAM MCHOVU, B12 NA DJ FETTY BAADA YA SAKATA YA KURUSHIANA MAKONDE NDANI YA STUDIO ZA CLOUDS NA KUFANYA HUARIBIFU

By on 12:04 AM

Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaana nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa nini ninachozungumzia mpaka sasa. Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 waliziweka ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio. Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta! 
Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa nataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn?
Baada ya massage nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani. Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi.....
PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS BAADA YA KUZICHAPA





Simu ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani, alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea na simu!!

Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani..
Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi, vifaa mbalimbali vya studio vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC, COMPUTER Meza nk. Endelea Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani watachukuliwa watangazaji hawa kwa kukosa utovu wa Nidhamu....

Thursday, July 3, 2014

LULU AANIKA ‘UPAJA’ KUWATEGA WANAUME

By on 9:31 PM
Stori:Mussa Mateja
GAUNI alilovaa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael hivi karibuni alipokuwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu limeonesha kuwatega wanaume hasa wakware kufuatia kuuanika ‘upaja’ wake.
Msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa kaachia 'upaja' wake.
Akiwa ndani ya Ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar, Lulu alionekana amevalia gauni refu lakini pembeni likiwa na mpasuo mkubwa ambapo kila alipokaa, mapaja yake yalionekana wazi hivyo kumfanya ahangaike kuyaficha huku wanaume nao wakitumia muda mwingi kumkodolea macho kisha kunong’ona.
“Duh!Haka kabinti kazuri na lile gauni alilovaa ndiyo anawaacha hoi sana wanaume,ile ni kututafuta ubaya na kama ni kututega kafanikiwa kwa silimia 100,” alisikika kijana mmoja akisema.
Paparazi wetu alifanya jitihada za kutaka kuongea na Lulu juu ya mpasuo huo, lakini hakuwa tayari na hata baada ya zoezi la utoaji wa tuzo, aliondoka fasta akiwa na wapambe wake.

PICHA ZA KIPIGO CHA DIDA ZAVUJA

By on 9:30 PM

Stori: Shakoor Jongo
Picha zinazoonyesha jinsi mtangazaji wa kituo cha Redio cha Times, Khadija Shaibu alivyochezea kichapo kutoka kwa mumewe, Edzen Jumanne zimevuja.
Majeraha katika mwili wa Dida baada ya kipigo kutoka kwa mumewe Ezden.
Picha hizo zinamuonesha Dida akiwa na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mkononi, kichwani na mapajani.
Dida.
Akizungumzia kipigo hicho hivi karibuni, Dida alidai kuwa, baada ya kutofautiana kufuatia wivu wa kimapenzi, mume wake huyo baada ya kumporomoshea mitusi, alichukua mkanda wa suruali na kumpiga nao hadi kumsababishia majeraha hayo hali inayomfanya muda mwingi avae kininja kuficha aibu.
Dida akionyesha majeraha aliyoyapata.
Mpaka sasa wawili hao kila mmoja kivyake huku ndoa ikielezwa kuwa haipo tena.

JOKATE : AKU, SIJAVUNJA NDOA YA DIDA

By on 9:29 PM

Stori: Hamida Hassan
Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’ amefunguka kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’ kwani ni mshikaji wake na wanaheshimiana.
Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
'Dida' akiwa na Ezden.
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi hata siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni mshikaji wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”
credit....  gp