Na Elias Msuya, Mwananchi
- Mmiliki wa biashara hiyo asema alifanya hivyo kuwasaidia kwa kuwa wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.
Pengine takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) kwamba
watoto wapatao milioni 250 wanatumikishwa katika ajira mbalimbali
duniani kote, zikawa ndogo kulingana na hali halisi kwa kuwa kila
kukicha, mapya huibuka.
Ajira hizi zinapaswa kupigwa vita kwa kuwa siyo tu
zinawanyima haki za msingi watoto, bali zinachochea umaskini kwa
familia na taifa kwa jumla.
Hassan Abdallah mkazi wa Tabata ni mmoja kati ya
wanaoshiriki katika biashara hii haramu ya kuajiri watoto. Hivi sasa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuajiri watoto 11 kwa kazi
za kuuza vitumbua huku akiwahifadhi ndani ya chumba kimoja.
Kati ya waajiriwa hao, watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wako wanane.
Katika makazi hayo, watoto walimwonyesha mwandishi
wa habari hizi banda la mabati wanalotumia kwa malazi likiwa kando ya
nyumba ya mwajiri wao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisukuru,
Lukresia Msuya anasema kuwa Abdallah na mkewe Fatuma Shomari wamekuwa
wakiwafuata watoto hao mikoani na kuwaleta jijini Dar es Salaam
kuwatumikisha kuuza vitumbua mitaani.
“Tulipigiwa simu juzi na katibu wa CCM wa mtaa
akisema kuwa kuna jambo la muhimu. Hapo ndipo aliponionyesha nyumba hii
ambayo ina watoto wanaotumikishwa kuuza vitumbua. Tukawakusanya na
kuwapelekapolisi,” anasema Msuya.
Amewataja watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo kuwa
ni pamoja na Furaha Samuel, Steven Tudius, Amani Adison, Yusuf Simon,
Richard Zakaria, Kackson Jackson Michael, Elia Wilson, Boniface
Lawrence, Baraka Francis, Zamda Yumpunju, Jema Ramadhani na Haji
Ramadhani.
Msuya amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo,
walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kisukuru kisha kuhamishia
shauri hilo Stakishari ambako Abdallah aliwekwa ndani.
“Nikiwa kama mzazi inaniuma kuona watoto hawa
wadogo wenye umri kati ya 17 na 12 wakifanyishwa kazi kama hizi.
Nawaomba wazazi wawakumbatie watoto kama vifaranga vya kuku. Mtoto wa
miaka 12 umfanyishe kazi, halafu utamlipa nini kama siyo kumdhulumu?”
alihoji.
Jinsi walivyokamatwa
Akieleza jinsi alivyogundua suala hilo, katibu wa
CCM wa Mtaa wa Kisukuru, Thomas Matiku anasema kuwa alipewa taarifa na
wananchi wakati akitoka Buguruni.
0 comments:
Post a Comment