Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Slaa amefika
Msikiti wa Mtambani kutoa pole kwa waumini na viongozi wa msikiti kwa
niaba ya chama kutokana na tukio la moto lililotokea juzi jioni.
Katibu Mkuu ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani,
Prof. Abdalah Safari mbali ya kutoa pole pia alipata fursa ya kuzunguka
maeneo mbalimbali kujionea madhara ya ya moto huo ambao hadi sasa kwa
mujibu wa Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam unakadiriwa
kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zenye thamani ya Tshs. Mil. 600.
Baada ya kuambiwa na Shehe Katimba mahitaji ya dharura kwa wakati huu,
Dk. Slaa aliguswa na suala la wanafunzi wa Seminari ya Mvumoni kukosa
vitu muhimu kwa ajili ya masomo yao hasa walioko Kidato cha Nne ambao
wanajiandaa na mitihani yao ya kuhitimu, ambapo aliomba apewe tathmini
ya mahitaji kwa wanafunzi hao ili chama kiweze kushirikiana na shule na
wadau wengine kuwasaidia waendelee na masomo!
Katibu
Mkuu akiwasikiliza wenyeji Shehe Rajab Katimba, Mkuu wa Seminari na
Mvumoni, Maalim wa Msikiti wa Mtambani na Katibu wa Msikiti alipofika
kutoa pole na kujionea athari!
0 comments:
Post a Comment