Friday, August 15, 2014

Diamond Amchana Wema Sepetu….Adai kuchoshwa na tabia yake ya kuwa na mashoga Wapenda Anasa na Wanywa Pombe

By on 9:09 AM

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemtupia vijembe mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram  akionekana kuchukizwa na tabia ya staa huyo kupenda maisha ya starehe zisizo na faida.
 

Katika ujumbe huo, Diamond ameandika kuwa angewaona mashabiki wa mrembo huyo wana akili na mapenzi ya dhati kama wangemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na kuacha starehe zisizo na faida na kutumia fedha kufanya mambo ya maendeleo kuliko kuvifaidisha viwanda vya kutengeneza pombe.

WEMANADIAMONDi
HUU  NDO  UJUMBE  WAKE:


“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…
 
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! 
Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel
Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel


Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!
dio

0 comments:

Post a Comment