DEREVA wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria
kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi
wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo
kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini
na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva
huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha
chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe
walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu
baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa
kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao, mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.
Tunashauri madereva kuwa makini na watiifu pindi wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa zikitokana na uzembe wa madereva kwa kutotii sheria za usalama barabarani-Mhariri.
JIUNGE NA GURUDUMU KWA KULIKE PAGE
0 comments:
Post a Comment