Mtu
mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya
kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema kijana huyo mwanamume
amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika
Kituo cha Polisi Chalinze.
Alisema
askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya
katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye maandishi
hayo.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu msaidizi, Athumani Mwambalaswa
amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa na
kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.
Hata
hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa kijiji kipi
kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta ndugu
zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado
hakijajulikana
0 comments:
Post a Comment