WATU
wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel
Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia
alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti.
<<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE HAPA>>
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Camillius Wambura alisema Ndahani aligongwa
na gari isiyofahamika kwa
kuwa lilikimbia baada ya ajali hiyo.
Alisema Ndahani alikuwa akitaka kuzuia
magari yasiukanyage mwili wa Onesmo Yarimunda aliyefariki dunia baada ya
kugongwa na basi la Prince Muro alipokuwa akivuka barabara.
Kamanda Wambura, alisema Yarimunda (36),
mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo aina ya Scania, juzi, saa 3
usiku maeneo ya Kibamba.
Maiti zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi
Kibaha. Dereva wa basi la Muro, Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha
anashikiliwa na polisi
0 comments:
Post a Comment