STAA
wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya tukio la
kihistoria kiasi cha kumliza mama yake mzazi, Sanura Kassim ambaye
alimwaga machozi kama mtoto mbele za watu.
Tukio la mama Diamond kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za Amani, juzi Jumatatu, mishale ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.
“Mipango yote ilifanywa kwa siri mama Diamond hakujua kilichoendelea. Diamond akiwa Marekani alitoa maelekezo mama yake afanyiwe shughuli hiyo hata kama hayupo kwa sababu siku ya kuzaliwa haijirudii,” alisema rafiki huyo.
Muda huohuo akafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari hilo lililopambwa ndani kwa vitu kibao vya thamani.
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA
Machozi ya mama Diamond hayakukoma hata baada ya kushuka ndani ya gari, alionekana kuchanganyikiwa kama siyo kutoamini sapraizi ya mwanaye, ndipo Miss Tanzania 2006, aliye pia mchumba wa mwanaye, Wema Sepetu na staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.
DIAMOND, WEMA NDOA LAZIMA!
Katika kuonesha kuwa sasa amekubali kwa dhati Wema awe mkwewe, mama Diamond aliapa lazima ahakikishe mwanaye anafunga ndoa na mlimbwende huyo.
“Hilo nataka mlijue kabisa. Nitafanya juu chini Diamond amuoe Wema maana ana roho nzuri sana. Niseme ukweli kuwa huyu msichana ndiye chaguo langu na wanaendana sana na mwanangu.
“Angalia wakiwa pamoja, mwanangu anapata mafanikio makubwa sana, nadhani nyota zao zinaendana hivyo sina pingamizi lolote. Ninachotaka ni kuhakikisha wanaoana,” alisema mama Diamond.
THAMANI YA GARI
Akizungumzia thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni 34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo kununuliwa.
“Hiyo milioni 34 ni pamoja na muziki unaouona ndani ya gari, hizi skrini tatu na mazagazaga mengine kama mnavyoona,” alisema Babu Tale huku akiwaonesha waandishi wetu.
DIAMOND BONGO
Hadi tunakwenda mitamboni, Jumanne usiku, ilielezwa kuwa, Diamond alitarajiwa kutua jana Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Marekani alipokuwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za BET.
Habari kutoka ndani ya familia zilieleza kuwa, nyota huyo naye ameandaliwa sapraizi ya nguvu kutoka kwa kampani yake wakishirikiana na familia. “Wamejiandaa vya kutosha kumfanyia saprazi ya nguvu na yeye mara tu atakapotua Bongo. Wanafanya siri sana, haijajulikana atafanyiwa nini,” kilipasha chanzo chetu.
Tukio la mama Diamond kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za Amani, juzi Jumatatu, mishale ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.
SAPRAIZI YA NGUVU
Waalikwa na mama huyo, wote walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Mmoja wa rafiki wa karibu na familia hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema kuwa hadi jioni, mama Diamond hakuwa akifahamu kuwa aliandaliwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
Waalikwa na mama huyo, wote walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Mmoja wa rafiki wa karibu na familia hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema kuwa hadi jioni, mama Diamond hakuwa akifahamu kuwa aliandaliwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
“Mipango yote ilifanywa kwa siri mama Diamond hakujua kilichoendelea. Diamond akiwa Marekani alitoa maelekezo mama yake afanyiwe shughuli hiyo hata kama hayupo kwa sababu siku ya kuzaliwa haijirudii,” alisema rafiki huyo.
KILICHOMLIZA
Muda mfupi baada ya shughuli ya kufuturu kukamilika, mama Diamond alishangaa kusikia kwamba kulikuwa na jambo jingine la ziada katika siku hiyo. Alitolewa nje huku akiimbiwa ‘happy birthday’ ndipo alipogundua kilichokuwa kikiendelea.

Mara
baada ya shampeni isiyo na kilevi kufunguliwa na waalikwa kupewa,
meneja wa Diamond, Babu Tale na wapambe wengine walimuongoza mama huyo
hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus Harrier na kuelezwa kuwa ni mali
yake kuanzia muda huo tamko lililomshtua na kuanza kulia akiwa haamini
alichosikia!Mama Diamond akilia huku kichwa kikiwa juu ya gari aliyopewa zawadi na mwanaye.
“Siamini
macho yangu, siamini... asante sana mwanangu (Diamond), nakuombea kila
kukicha mwanangu uwe na afya njema, unilee kwa upendo, asante Mungu,”
alisikika mama Diamond akitamka kwa sauti iliyoambatana na kilio cha
nguvu.Muda huohuo akafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari hilo lililopambwa ndani kwa vitu kibao vya thamani.
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA
Machozi ya mama Diamond hayakukoma hata baada ya kushuka ndani ya gari, alionekana kuchanganyikiwa kama siyo kutoamini sapraizi ya mwanaye, ndipo Miss Tanzania 2006, aliye pia mchumba wa mwanaye, Wema Sepetu na staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.
Mastaa
hao ambao ni mtu na shogaye, walimchukua mwanamke huyo na kwenda naye
pembeni ambako walimsihi atulie na akubaliane na alichokiona kwani
ndiyo ukweli wenyewe.
Juhudi zao zilizaa matunda, kwani muda mfupi baadaye mama Diamond alifuta machozi na kurudi katika hali yake ya kawaida ingawa alishindwa kuficha furaha yake.
Juhudi zao zilizaa matunda, kwani muda mfupi baadaye mama Diamond alifuta machozi na kurudi katika hali yake ya kawaida ingawa alishindwa kuficha furaha yake.
DIAMOND, WEMA NDOA LAZIMA!
Katika kuonesha kuwa sasa amekubali kwa dhati Wema awe mkwewe, mama Diamond aliapa lazima ahakikishe mwanaye anafunga ndoa na mlimbwende huyo.
“Hilo nataka mlijue kabisa. Nitafanya juu chini Diamond amuoe Wema maana ana roho nzuri sana. Niseme ukweli kuwa huyu msichana ndiye chaguo langu na wanaendana sana na mwanangu.
“Angalia wakiwa pamoja, mwanangu anapata mafanikio makubwa sana, nadhani nyota zao zinaendana hivyo sina pingamizi lolote. Ninachotaka ni kuhakikisha wanaoana,” alisema mama Diamond.
THAMANI YA GARI
Akizungumzia thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni 34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo kununuliwa.
“Hiyo milioni 34 ni pamoja na muziki unaouona ndani ya gari, hizi skrini tatu na mazagazaga mengine kama mnavyoona,” alisema Babu Tale huku akiwaonesha waandishi wetu.
DIAMOND BONGO
Hadi tunakwenda mitamboni, Jumanne usiku, ilielezwa kuwa, Diamond alitarajiwa kutua jana Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Marekani alipokuwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za BET.
Habari kutoka ndani ya familia zilieleza kuwa, nyota huyo naye ameandaliwa sapraizi ya nguvu kutoka kwa kampani yake wakishirikiana na familia. “Wamejiandaa vya kutosha kumfanyia saprazi ya nguvu na yeye mara tu atakapotua Bongo. Wanafanya siri sana, haijajulikana atafanyiwa nini,” kilipasha chanzo chetu.
Mama Diamond, Bi. Sanura akimlisha keki 'mkwewe' Wema Sepetu katika sherehe yake ya kuzaliwa.
DIAMOND ANATISHA
Nyota ya Diamond imeonekana ikiwaka sana siku za hivi karibuni ambapo amekuwa akipiga shoo za mara kwa mara katika nchi mbalimbali huku akishirikishwa kwenye tuzo za ndani na za kimataifa.
Si jambo la ajabu kusema kuwa, Diamond kwa sasa ndiye Mwanabongo Fleva anayefanya vizuri zaidi pengine kuliko wote katika muziki huo – MHARIRI.

0 comments:
Post a Comment