Afisa
Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi
wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana
Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini
kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela.
Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikali – WHVUM
Tafiti
zilizofanywa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania zinaonyesha kuwa
maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia
asilimia 5.1 kwa mwaka 2011/2012 ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na
asilimia 3.8 ni wanaume.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela jana katika Viwanja vya
Sabasaba alipokutana na waandishi wa Habari katika banda la TACAIDS
kuwaelezea hali halisi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Dr.
Kamwela amesema kuwa TACAIDS imekua ikifanya ukaguzi wa tafiti
(takwimu) zilizokusanywa katika maeneo mbalimbali nchini na kuzitathmini
tafiti hizo kama zina viwango wakiwa na lengo la kupanga mikakati
itakayowawezesha kuelekeza rasililmali ili kuondoa maambukizi mapya
yanayoweza kujitokeza.
Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba
jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS
Bw. Godlease Malisa.
“Tafiti
zinaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi kwa asilimia 14.7 ambapo Iringa ina asilimia 9.1 ya watu
walioathirika na Virusi vya Ukimwi na Mbeya ikiwa na asilimia 9, kwa
upande wa mikoa yenye kiwango cha chini cha maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi ni Manyara na Kilimanjara ikiwa na asilimia 2 ya maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi” amesema Dr. Kamwela.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ambazo TACAIDS imekua ikizipata katika ukusanyaji wa
takwimu za watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini Dr. Kamwela
amesema kuwa uhaba wa wataalamu, uhaba wa vyuo vinavyofundisha taaluma
ya ufuatiliaji na tathmini pamoja na uhaba wa fedha kwaajili ya
kufuatilia na kutathimini hali halisi ya maambukizi ya Ukimwi nchini
vimekua vikizuia malengo ya kutokomeza Ukimwi nchini.
Kwa
upande wake Afisa Mawasiliano kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa
amesema kuwa TACAIDS imekuja na mkakati unaozingatia sifuri tatu (three
zeros) ukiwa na maana sifuri ya kwanza maambukizi mapya ya Virusi vya
Ukimwi yashuke hadi sifuri, huku sifuri ya pili ikimaanisha unyanyapaa
dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi upingwe hadi sifuri na
sifuri ya tatu ikimaanisha maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto
yapunguzwe hadi sifuri.
Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela kati akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Ufuasihii
wa dawa na huduma za jamii wa ICAP Globali Health Action Bi: Agnes
Rubare Rwegasha alipotembelea banda la ICAP, kushoto ni Afisa
Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa.
Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population
Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo
katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva
Matemu)
0 comments:
Post a Comment