Akisimulia tukio zima kwa majonzi, mjane wa marehemu Aisha Amir (75) alisema, ameumia sana kumpoteza mume wake kipenzi ambaye anadai kukatishwa uhai na mpwa wake aliyemtaja kwa jina moja la Sabata aliyemshambulia na kumvunja shingo.
“Siku
ya tukio tulikuwa tumelala mimi na mume wangu, ghafla tukaona mwanga
wa tochi, tulipofuatilia tukagundua ni Sabata, nilipomwambia anataka
nini, akatishia kuniua. Alisema nikae kimya.
“Alimwamrisha marehemu aamke ili ampe chipsi na soda alizomletea lakini alikataa kutokana na hali yake kiafya kuwa mbaya. Alipoona amekataa, alimsukuma chini kwa nguvu, mzee akaanza kulia akilalamikia maumivu makali ya shingo. Tukiwa tumeduwaa, Sabata alianza kumwagia haja ndogo usoni,” alisema Bi. Aisha akimwaga machozi.

“Hata hivyo alifanyiwa matibabu na kuruhusiwa, akaonekana kuwa na hali ya kuridhisha kabisa, hadi hali yake ilipobadilika nyumbani na kufariki,” alisema Bi. Aisha.
Naye mtoto wa marehemu, Seleman Halfan alisema muda mfupi kabla ya baba yake kufariki, alikuwa akilalamika kuuawa na mpwa wake Sabata.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Chalinze kisha kupelekwa mahabusu katika Gereza la Mifugo la Ubena, Chalinze mkoani hapa akisubiri hatua zaidi za kisheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Nesphory Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola dhidi ya watu wasio wema kwenye jamii.
0 comments:
Post a Comment