Licha ya elimu ya kampeni za
tohara katika wilaya ya kilolo kupokelewa na kuwa
na mwamko wa kujitokeza kwa watu kwa kiwango kikubwa katika zoezi
la kufanyiwa tohara bado kunachangamoto zinazowakumba watoa huduma katika
kituo cha kutolea huduma hiyo.
Akizungumza mwelimishaji rika
wa kampeni za tohara zinazoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la JPIEGO kutoka katika kituo cha afya
cha nzihi SCOLASITIKA MKWEMWA
amesema kuwa watu kuanzia 98 mpaka 99 hujitokeza kwa siku.
Amema kuwa,kuna wakati wamekuwa wakishindwa
kuwahudumia na kulazimika kusitisha huduma kutokana na kuwa jengo husika halina
umeme, kwani huduma hizo hufanyika hata nyakati za usiku.
Amesema kuwa wengi wao
wanapenda kupewa huduma hiyo mida ya usiku kwa ajiri ya usiri huku
akiitaja changamoto nyingine kuwa ni watu wanashindwa kujitokeza kutokana
na kuwa huduma hiyo inaambatana na zoezi la upimaji vvu.
Akizungumza meneja wa eneo
hilo DOLIC KADETE amesema kuwa
huduma ya tohara kwa kituo hicho huanza saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja
jioni.
Ameongeza kwa kutaja
changamoto nyingine inayowakabili ni kuwa asilimia kubwa ya watoto
wanaorudishwa kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya vidonda huwa haviko katika
hali nzuri.
Akizungumza mmoja wa
wanaume ambao wamefanyiwa tohara KASIANI SAFARI amelishukuru shirika la jpiego
kwa huduma hiyo huku wakiwashauri wanaume wengine ambao hawajafanyiwa tohara
kujitokeza kupata huduma hiyo kwani itawasaidia kuwakinga na magonjwa ya zinaa.
Kampeni za tohara zinafanyika
katika mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya vvu kiko juu na katika mikoa
ambayo tohara inafanyika kwa kiwango kidogo kuanzia miaka 10 na kuendelea Lengo
likiwa ni kusaidia kupunguza maambukizi ya vvu kwa asilimia 60.
Aidha kampeni za tohara ambayo
ni kuanzia mwezi wa tisa mwaka jana hadi mwezi wa tisa mwaka huu shirika la
jpiego lilipanga kuwafikia watu laki moja na ishirini na tano elfu na kufikia
mwezi huu wa saba tayari wameshafikia lengo.
0 comments:
Post a Comment