Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania imewaonya watu wanaojiita
madaktari na maprofesa bila ya kuwa na sifa hizo huku wakidai kuwa na
uwezo wa kutibu magonjwa yasiyotibika ukiwemo ugonjwa wa Ukimwi na
kisukari.
Mganga
mkuu wa serikali Dkt Donnan Mmbando ametoa onyo hilo jijini Dar es
Salaam jana, na kufafanua kuwa wenye haki ya kujiita hivyo kwa mujibu wa
sheria na kanuni zinazosimamia tiba asili na tiba mbadala nchini
Tanzania, ni wale tu wenye sifa zinazotambulika na mamlaka mbalimbali za
serikali.
Dkt
Mmbando amesema inashangaza kuona watu wakijitangaza na kujinadi eti ni
madaktari na wana uwezo wa kutibu magonjwa hayo na mengine ambayo
yameshindikana ilhali sio kweli bali ni njia za kijanja za kutaka
kujipatia pesa.
Aidha, Dkt Mmbando amesema katika kuhakikisha dawa za tiba asili na tiba mbadala zinatolewa kwa mujibu wa viwango vinavyotambulika kisheria, wizara inakamilisha taratibu kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa na jukumu la kusindika dawa zote za asili ili ziwe katika mwonekano na viwango vya kisasa.

0 comments:
Post a Comment