Friday, July 11, 2014

WAZIRI WA MAZINGIRA AKANUSHA KUTUMIA FACEBOOK YENYE JINA LAKE‏

By on 1:26 AM

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira, Dkt Binilith Mahenge.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo.
Waziri Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani hapo na kusema kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo vibaya kwa kufungua akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi kujiunga na facebook na hana mpango huo. 
Amesema kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu wanaoziamini taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo wakidhani zimetolewa na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si yeye.
 "Ukiangalia pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni uongo mtupu, kwa mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia ya kweli, hii inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri Mahenge.
 Aidha ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia jamii huku akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha kuwapotosha watu kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na atakayebainika sheria iko wazi dhidi yake. 
Hivi karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahadaa watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi
Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete
                              <<BOYA HAPA ULIKE PAGE KWA HABARI ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment