Wednesday, July 2, 2014

UPDATE: Jeshi La Polisi Iringa lakamata watuhumiwa wa Mwanafunzi Aliyechomwa Moto

By on 12:33 AM

Mwili wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO) umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.
Wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wa manispaa ya Iringa walioguswa na tukio hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya kuuga mwili huo ilifanyika.
Jeshi  la Polisi mkoani iringa   linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi wa duka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kihesa katika manispaa ya Iringa kwa tuhuma  ya kumchoma moto mwanafunzi  huyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa anawaka moto.
Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake
Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake
Mungi alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo   Jeshi la Polisi lilifika katika  eneo hilo  na kumkuta Daniel  Lema (25)  akiwa ameanguka chini huku akiwa amefungwa mikono nyuma.
Kamanda huyo aliwataja  watuhumiwa hao kuwa ni  Mussa Nganga (28), Costa Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote wakazi wa Kihesa.
“Tulipopata taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta ameanguka chini tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta akipumua kwa shida ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Alisema kuwa  mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa Inbox bar inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela akipata kinywaji huku akiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la dunia) ambayo inaendelea nchini Brazili.
“Mwanafunzi alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na baada ya mpira huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwako Kihesa kabla ya kufika nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo Glory lodge ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery  akaingia hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.
Alisema wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge  ambae ni mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia na baada ya kukimbia alimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia kitendo kama hicho.”alisema Mungi.
Baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu yake mpaka alipokutwa na mauti jana majira ya saa nane mchana.

Tuesday, July 1, 2014

DIAMONDO AWATIA KIWEWE NELLY,CHRISS BROWN NA WENGINE WAMAREKANI...JINSI SHUKA NAYO HAPA

By on 10:57 PM

Stori: Andrew Carlos na Musa Mateja
Next level! Staa wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya kweli kimataifa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameandika historia kwenye Tuzo za Black Entertainment Television (BET) 2014 huku akiwatia kiwewe mastaa wakubwa kama Cornell Iral Haynes ‘Nelly’, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ na wengine kibao.
Diamond akipongezwa na Nelly
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre jijini Los Angeles, Marekani ambapo Diamond alikuwa ameteuliwa kuwania Kipengele cha Mwanamuziki Bora kutoka Afrika akiwa sambamba na mwanamuziki Davido (Nigeria), Mafikizolo (Afrika Kusini), Tiwa Savage (Nigeria), Toofan (Togo) na Sarkodie (Ghana).
TUZO YAENDA KWA DAVIDO
Tuzo hiyo haikuwa bahati kwa Diamond kwani ilikwenda kwa Davido.
Licha ya kukosa tuzo hiyo, yapo mengi ambayo Diamond ameweka historia au rekodi katika ‘event’ huku kuunganishwa na mastaa hao ikiwa topiki muhimu.
MCHUMBA WA CHRISS BROWN AMSHOBOKEA
Katika hali ya kushangaza, mwanamitindo maarufu Marekani ambaye ni mchumba wa Chris Brown, Karrueche Tran alionekana kumshobokea Diamond mara alipokutana naye uso kwa uso.
Karrueche alijikuta hajiwezi alipokuwa  akimhoji Diamond ambapo moja kwa moja alimvutia kipaza sauti na kuanza kumpiga maswali huku akionesha kuvutiwa naye kwa muonekano aliokuwa nao.
.....akihojiwa na demu wa Chris Brown.
Karrueche alikuwa akijichekeshachekesha huku akimhoji kuhusiana na mwanamuziki ambaye Diamond anamkubali ambapo alijibu ni Chris Brown, wote wakajikuta wakiangua kicheko.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Karrueche muda wote aliendelea kumshangaa na mwisho wa siku wakabadilishana namba za simu.
MASTAA MACHO JUU
Ulipofika wakati wa utoaji tuzo katika kategori ya Mwanamuziki Bora kutoka Afrika, lilipotajwa tu jina la Diamond kutoka Tanzania na wimbo wake wa Number One RMX, mastaa kibao walionesha kushangaa na ndipo macho yote yakahamia eneo aliokuwa amekaa.
Wengi walionekana kutoa maneno ya chinichini sambamba na kumuoneshea vidole wakionesha kumkubali kwa kutinga mjengoni hapo.
NELLY, CHRIS BROWN WAINGIWA KIWEWE
Wakati Diamond anaingia ukumbini, mastaa mbalimbali duniani walionekana kumshangaa na kati yao alikuwa ni Nelly ambaye aliushikilia mkono wa Diamond kwa sekunde kadhaa akitaka waendelee kupiga stori.
Diamond akiwa kwenye pozi
Wakiwa katika zulia maalum jekundu, Nelly aliyewahi kutamba na wimbo wake maarufu wa Dilemma alionekana na kutaka kumfahamu zaidi Diamond.
Kila sehemu aliyokuwa akienda, Nelly hakutaka kumuacha na alionekana kuambatana naye kwa kumng’ang’ania mkono kila kona akipiga naye picha na kuzunguka eneo lote wakiwa pamoja.
Naye Chris Brown ambaye aliangusha bonge la shoo alionekana kumshangaa Diamond huku akitamani kuendelea kukaa naye.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ukumbini humo, maswali mengi yaliibuka kuwa iweje, kwa Mtanzania kama yule kukanyaga katika mjengo mmoja na mstaa wa dunia.
TYSON, MAYWEATHER WADUWAA
Mabondia maarufu duniani akiwemo Floyd Mayweather na Mike Tyson walijikuta wakiduwaa kwa kumshangaa kwa kila hatua aliyokuwa anapiga. Macho yao hayakuwa mbali naye na hata katika zulia jekundu, Maywearher, baada ya kumaliza kupiga picha akiwa na mkewe alimfuata Diamond na kuongea naye mawili-matatu kuonesha kukumkubali.
MASTAA KIBAO WAGOMBEA NAMBA
Wakati shoo hiyo ikiendelea baadhi ya msataa waliokuwa pembeni na  Diamond walionekana kumfagilia na hata wengine kuomba namba za simu kwa malengo tofauti ikiwa ni pamoja na kutaka kufanya naye kolabo katika siku za usoni.
Cornell Iral Haynes ‘Nelly’, akiwa kwenye pozi
LUPITA, DIAMOND USO KWA USO
Staa kutoka Kenya ambaye anatingisha katika soko la filamu za Hollywood, Marekani kupitia filamu ya 12 Years A Slave, Lupita Nyng’o alikutana uso kwa uso na Diamond wakiwa wote wametokea Ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Walionekana kuwa na furaha kwa pamoja na ikumbukwe kuwa Lupita amejizolewa umaarufu mkubwa ambapo hata Jay-Z na Rihanna waliwahi kuandika kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii wakioneshwa kumkubali kwa kazi zake.
Mastaa wengine wakubwa aliokutana nao ni pamoja na Ashanti, DJ khalid, Jeniffer Hudson, French Montana, John Legend, Paris Hilton na wengine kibao
HABARI NYUMA YA PAZI
Duru za kibahari zilieleza kwamba mambo yote yanayokea kwa Diamond kuna nguvu kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye hivi karibuni alimkutanisha mtoto huyo wa Tandale na meneja wa wanamuziki wakubwa duniani, Tremaine Neverson ‘Trey Songz’ na Sean Michael Leonard Anderson ‘Big Sean’, ili kufanya nao kazi.
“Siyo jambo rahisi na bado milango itazidi kufunguka zaidi kwani JK aliahidi kumsaidia. Kwa kuunganishwa na mastaa wakubwa duniani sasa hivi utasikia amehamia Marekani kutusua mtonyo,” alisema mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva ambaye naye anafanya vizuri.
Christopher Maurice ‘Chris Brown’ akiwa kwenye pozi
Akizungumza na mwanahabari wetu kutoka jijini Los Angeles, Diamond alisema kuwa hakuamini jinsi alivyopokelewa na mastaa wakubwa ambao hakutarajia kukutana nao uso kwa uso.
“Sasa najua ndoto itatimia. Mastaa wakubwa lakini wamenionesha upendo wa ajabu. Naona wasanii wote duniani wanapendana sana. Jamaa hawana ubaguzi. Walinichangamkia sana utadhani tunafahamiana.
“Kuna mengi nafanya nao lakini siwezi kuwataja kwa sababu si unawajua Wabongo?
“Lakini nikidondoka tu Bongo naachia video mbili kali sana, mashabiki wangu wasikilizie.
“Kuhusu kukosa tuzo, mimi naona ni mwanzo mzuri. Inanipa hasira ya kutengeneza muziki mzuri utakaopendwa na watu wengi duniani. Tusikate tamaa, ni mwanzo mzuri. Pia asiyekubali kushindwa si mshindani,” alifunguka Diamond akimshukuru Mungu kwa yote anayomtendea kila kukicha kisha watu wanampa sapoti.
Mike Tyson akiwa kwenye pozi
SASA LEVO ZA AKINA HASHEEM THABEET
Kwa sasa Diamond anakuwa ni staa mwingine wa Kibongo wa kimataifa akitanguliwa na staa wa NBA, Hasheem Thabeet, Modo Flaviana Matata na wengineo.
CREDIT:GP  
 <<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>

MHADHIRI MWANDISHI WA CHUO KIKUU CHA MTAKATIKU AUGUSTINE TANZANIA (Saut), NKWABI NG’WANAKILALA AZIKWA

By on 6:53 AM

MHADHIRI Mwandamizi Idara ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (Saut), Nkwabi Ng’wanakilala,  amezikwa leo katika shamba lake lililopo Kibamba-Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Marehemu alifariki dunia Juni 28 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa Bugando alipokuwa akitibiwa baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na utumbo kujikunja.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
credit...GP
                        <<KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE>>

Monday, June 30, 2014

Msajili wa vyama vya Siasa amzuia Mbowe kugombea tena uenyekiti CHADEMA

By on 1:51 PM

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.
“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo