Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui
kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila
kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu
wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa
kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda
kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya
6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa
chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha
mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa
uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo,
akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa
alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni
wilaya na mkoa.
“Mjadala kuhusu ukomo wa
uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao
halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao
vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya
chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama
hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye
sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa
kazi.
“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba
aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua
hiyo
0 comments:
Post a Comment