Watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga risasi
moja ya kichwani mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Busambala
wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 60
huku kichwa chake kikisambaratishwa kabisa na risasi hiyo.
Mauaji
hayo ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia jana,baada ya
majambazi hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi
huyo na familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa
bapa za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika
kuwapa kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka katika
taasisi moja ya fedha.
Afisa
upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara ACP Rogati
Mlashan,akizungumza toka eneo la tukio, amesema baada ya majambazi hayo
kuvunja milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi tatu na moja
kumpata kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia papo hapo na
kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo ili kuhakikisha
wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi wa serikali katika kata ya
Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao
baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM,wameliomba
jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao utawezesha kukamatwa kwa
wahusika,hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa
waliyonayo sasa.
0 comments:
Post a Comment