Friday, August 29, 2014

Utafiti: Wanawake Wanene ni Mafundi Jikoni Kuliko Wembamba

By on 9:16 PM

Duniani kuna tafiti nyingi na mara nyingi wataalamu wa masuala mabalimbali huja na tafiti tofauti tofauti...

Moja ya tafiti ambayo imenivutia kiasi cha kuja hapa jamvini ni utofauti wa ufundi wa jikoni baina ya mwanamke kimbaumbau na yule mwenye neema za allah "curvaceous" ...

Inaaminika kwamba manawake wenye nyama za nyongeza 'curvy girls' wana ujuzi mkubwa wa mapishi kuwazidi wale ambao miili yao ni vimbaumbau...

Sababu kubwa haswa inayopelekea kuwepo kwa dhana hii ni kutokana na utofauti wa tabia za ulaji baina ya mwanamke tipwatipwa na kimbaumbau...

Wataalamu wanadai eti kwa kuwa wanawake vimbaumbau ni wavivu sana kula basi hata ujuzi wao wa kuandaa madikodiko, mahanjumati na mazagazaga ni mdogo pia...(hawa nafikiri ndio wale wanaochemsha nazi bila hata kuikuna)...

Hivyo wito wangu kwetu vidume haswa wale mnaotafuta waifu matirio, kama wewe ni mtu wa kuchunuku zagazaga hebu konsida basi hiki kigezo usijekuwa walazwa na njaa au kutwa washinda kwa mama muuza...

0 comments:

Post a Comment