1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.
Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku atachoka, maana hana moyo wa jiwe bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na kupendwa katika maisha yao.
Imeandaliwa na www.tabasamunafuledi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment