MSANII
wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Nasseb
Abdul ‘Diamond’, ni miongoni mwa wanamuziki ambao kila siku lazima
usikie habari zao kwenye vyombo vya habari.
Habari
za Diamond pamoja na mafanikio mbalimbali anayoyapata, ambayo amekuwa
akiandikwa katika muziki, pia ya kuvutia na yanayofanya asomwe,
kusikilizwa na kutazamwa zaidi, ni masuala ya kujihusisha kwake katika
mapenzi na wasichana mbalimbali, tena wenye majina makubwa katika sanaa.
Hadi
mimi mzee wa Tamu Tamu ninapoandika makala hii, msanii huyu tayari
ameshakuwa na mahusiano na Wema Sepetu (Miss Tanzania 2006, ambaye hivi
sasa ni mcheza filamu), Jokate Mwegelo (Miss Tanzania namba mbili mwaka
2006 na mwanamitindo), Jackline Wolper(mwigizaji mkongwe wa Bongo Muvi)
na Peniel Mungilwa ‘Penny’ (mtangazaji wa runinga DTV). Katika mahojiano
ya hivi karibuni na kipindi cha ‘Take One’, Diamond aliweza kufunguka
kuhusu mahusiano yake na wasichana hao, mmoja baada ya mwingine na
kueleza ni namna gani alikuwa nao na sababu za wengine kujikuta
akiwabwaga bila huruma.
WEMA SEPETU
Diamond
anasema, Wema alianza naye mahusiano baada ya kubwagana na mpenzi wake
aliyemtaja kwa jina moja la Sarah, ambaye anadai alimpenda mno, lakini
akaja kumfanyia kitu ambacho hatakisahau maishani mwake.
Ni kutokana na kutendwa huko, akajikuta anaimba wimbo wa ‘Nenda Kamwambie’ na ‘Mbagala’, zote zikiwa zinamlenga msichana huyo.
Anadai,
alihamishia penzi kwa Wema, kwani mbali na kumpenda, pia alikuwa
akifanana kwa kiasi fulani na Sarah na kuona kama kapata mbadala wa
kumtuliza mawazo na katika kuonesha hilo, alijikuta kila wakati akiwa
anamwambia Wema namna gani anavyofanana na msichana huyo, jambo ambalo
lilikuwa likimletea kero kwa namna moja au nyingine na Wema.
Hata
hivyo, Diamond anasema kwamba wakati akiwa katika penzi hilo zito,
wakati huo huo Wema alikuwa ana mwanamume mwingine, lakini kwa kuwa
alikuwa akimpenda, walikubaliana na maisha yakawa yanaenda, japokuwa
wakati alipokuwa akimuaga kwamba leo anakwenda kulala kwa mwenzake, roho
ilikuwa ikimuuma sana, lakini alishindwa la kufanya, kwani inzi kufia
kwenye kidonda ni jambo la kawaida.
“Jamani,
hapa naomba nieleweke kuwa si kwamba nilimkubalia Wema kwa kuwa labda
mwanamume huyo alikuwa na hela, la hasha, bali ni mapenzi niliyokuwa
nayo kwa binti huyo, japo tulikuja kutibuana na kuamua kuachana naye
alipoingiza mwanamume mwingine wa tatu, ambapo nilishuhudia hadi
‘message’ zake kwenye simu, nikaona asije kuniua bure na maradhi,”
anasema.
Akizungumzia
kuhusu filamu wanayotarajia kuicheza na Wema siku za karibuni, Diamond
anasema mara ya kwanza ilikuwa vigumu kukubali kutokana na utofauti
waliyonayo hivi sasa na mrembo huyo, lakini baada ya maongezi ya muda
mrefu na waandaaji na fedha ya maana ambayo wameahidi kumlipa, akajikuta
anakubali kucheza. ‘Mpunga’ ambao anadai hajawahi kulipwa tangu aingie
kwenye fani ya muziki.
JOKATE MWEGELO
Diamond
anaendelea kusisitiza kwamba, alikuwa na mahusiano na Jokate, japokuwa
dada huyo hajawahi kujitokeza kukanusha au kukataa habari hizo.
Anamsifia
mrembo huyo kwamba alikuwa mpole na mnyenyekevu na anayejiheshimu, japo
alikuja kumuacha pale alipoamua kurudiana na Wema, kitu ambacho mpaka
leo hajui ni kwa nini alimuacha na kuhisi labda alirogwa.
“Yaani
huyu dada ni kati ya wanawake ambao najutia kuwakosea hapa duniani na
sijui nifanye nini, ili ajue kwamba najutia maamuzi yangu, kwa kuwa
nilimtenda mno, ukizingatia kwamba hakuna alichonikosea,” anasema
Diamond.
PENNY
Penny
ambaye anadaiwa kuwa alikuwa ni rafiki wa karibu wa Wema, Diamond
anadai kumpenda kutokana na kuwa na sifa za mwanamke anayemtaka.
Kutokana
na mapenzi anayoyapata kwa dada huyo, anasema kwamba ni mwanamke
anayeamini ataishi naye muda mrefu, kwani mpaka sasa hivi hajaona
mapungufu yake na amekuwa muwazi sana kwake kwa kila jambo analolifanya.
Kuhusu namna alivyopokea taarifa ya kucheza filamu moja na Wema, awali
anadai ilikuwa vigumu kumuelewa, lakini baada ya kumpa somo na
kumuelewesha namna itakavyomuingizia fedha, Penny alimuelewa.
Kwa nini anapenda wanawake ‘masupa staa’?
Hapa, Diamond anabainisha kuwa si kwamba anawapenda, ila inatokana na kazi zake kumkutanisha na wanawake wa aina hiyo.
“Unajua
mimi hata nikienda kupiga shoo mahali au kufanya ‘interview’,
nikishamaliza pale ni kuingia kwenye gari langu na kurudi nyumbani au
kuendelea na shughuli nyingine za kikazi, kwa hiyo unakuta wanawake
ninaokutana nao ni wa aina hiyo unayosema na mimi kama mwanamume,
nimeumbwa na moyo wa kutamani na kupenda jamani, ndivyo inavyonifanya
niwe hivyo,” anasema.
WOLPER
Huyu anafahamika sana kuwa ni msanii
wa Bongo Muvi na ni moja wapo ya wanawake wazuzi sana ambaye kila
mwanaume anatamani kumvua chupi na kumuonja japo kidogo! Mzee mzima
Diamond ashaapitia kitaaambo tunavyoongea hapa!
Diamond anadai kuwa mwanamke huyu
hakudumu naye sana kwani alimla si zaidi ya mara nne. Aliongezea kuwa
alimlamba tu by the way kwa sababu alijipendekeza kwake walipokuwa
wakikutana katika kumbi za starehe, na hivyo kumfanya kuonesha uwanaume
wake kwa kumvua chupi mwanamke huyo!
Mafanikio
Katika
mafanikio, mbali na kuwa msanii anayelipwa fedha nyingi katika shoo
hapa nchini, kwenye akaunti yake anadai ana sh milioni 100 na ushei hadi
sasa, ambazo mara nyingi hapendi kuzigusa.
0 comments:
Post a Comment