Thursday, May 1, 2014

MAPENZI YA KUIBA RAHA SANA,SOMA MKASA HUU WA KUSISIMUA KIMAPENZI MTU ANAVYOWEZA KUSALITI NDAO YAKE:

By on 8:19 PM

Mkasa wa Lauryn (si jina lake halisi), ni somo kwako namna mtu anavyoweza kusaliti ndoa. 


Mara nyingi tego la usaliti huanza taratibu kama utani, ukiliruhusu hutawala na kukutesa kihisia, usipoyashinda hayo mateso hujikuta unaangukia dhambini.
Lauryn aliisababishia ndoa yake misukosuko mingi. Kosa kubwa alilolifanya ni kutoka kimapenzi na kijana Paul aliyekuwa mpangaji mwenzake. Katika mfululizo wa simulizi yake, anaelezea jinsi alivyoanza kutengeneza ukaribu na Paul hadi kuvunja katazo la amri ya sita.

 “Mchana nilipika chakula, nikamtumia SMS Paul aje kula, akanijibu kazi ni nyingi saluni. Nilijisikia vibaya lakini usiku tulipata muda mwingine mzuri. Maana baada ya chakula cha jioni (dinner), mimi na Paul tulibaki sebuleni tukizungumza lile na hili. Alitaka kuanza ule mchezo wa kuzomea, sikumpa ushirikiano.

“Aligusisha paji lake la uso kwenye la kwangu, bado sikumpa ushirikiano wowote. Sikutaka michezo, nilitaka tufanye kweli. Ndiyo maana nilipoona analeta yale mazoea ya kuzomeana sikumpa ushirikiano. Naye alipoona simpi ushirikiano, ikabidi ajiongeze na kutimiza kile nilichotaka.

“Kwa kutumia kinywa chake, aliitumbukiza midomo yangu ndani yake, kwa hatua hiyo nilimpa ushirikiano wa kutosha. Tulibadilishana kila ambacho iliwezekana kupitia vinywa vyetu. Nilisikia burudani hasa ila niliendelea na tabia yangu ya kumtegea Paul ndiye atangulie mbele nifuate.

“Kwa maana hiyo nilitamani tusiishie kwenye kiss peke yake, nilitaka mikono yangu ifanye utalii kwenye maeneo yote muhimu ya Paul, vilevile na yeye apitishe mkono wake katika kona tofauti za mwili wangu. Nilitamani anishike maeneo mengi lakini sikuthubutu kumuomba afanye hivyo na nilijizuia kumshika popote.
“Hatimaye Paul alifika pale nilipopataka, aliuruhusu mkono wake wa kushoto kufanya utundu kwenye mwili wangu. Wakati huohuo midomo yote iliendelea kung’ang’aniana. Ulimi wangu ulikuwa ukigeuzwageuzwa kinywani kwa Paul. Ni mfyonzaji mzuri. Nilifurahia kila kitu.

“Nami nilianza kutalii kiwiliwili cha Paul. Nilipeleka mkono kila palipohusika. Katika maeneo yenye mshawasha, yale yaongezayo muwasho, niliweka mkazo kidogo. Tulipashana joto bila woga wakati pale tulikuwa sebuleni na mume wangu alikuwa chumbani amelala.

“Jinsi tulivyopashana joto ndivyo mabadiliko yalivyotokea, kiwango cha upumuaji kwa kila mmoja kilibadilika. Nilipata raha ya ajabu na kwa mshangao, nilishtukia nafika katika mshindo, yaani nilifika kileleni kwa ile michezo tu, kabla hata mchezo wenyewe haujafanyika.

“Baada ya kuona hivyo, nilimsukuma Paul, nikakimbililia msalani kujisafisha. Nilirudi pale sebuleni, nikanyoosha mikono, naye akanisogelea, tukakumbatiana, nilimkisi na kumshukuru. Nadhani hata yeye hakujua kwa nini nilimshukuru, maana sikumfafanulia. Ukweli ni kwamba nilimshukuru kwa kunifikisha kileleni bila mechi yenyewe kuchezeka.

“Baada ya shukurani, nilienda zangu chumbani kulala. Huko nilimpa mume wangu mgongo, nilipitiwa na usingizi mzito kwa maana nilijisikia mwepesi sana baada ya ile hali iliyonitokea. Wanasema sikio la kufa halisikii dawa, kesho yake tena mambo yakawa mengine. Hakika siwezi kumsahau Paul.

“Paul ni kijana, mambo yake yote ni ya ujanaujana. Mavazi yake na hata wanawake aliowahi kuwa nao nami nikawashuhudia ni warembo ambao mavazi yao ni ya kileo. Suruali, vimini, vitopu ndiyo mapigo yao.


“Kwa kawaida Paul ni mtu anayejipenda kweli ni kama vijana wengi wa saluni walivyo. Huvaa jeans, mashati au hata fulani nzuri sana. Siku zote huwa anapendeza, na haya ni mambo mengine yaliyonivuta kwake japo si kwa asilimia 100.
 
“Ukweli ni kuwa kilichonifanya kufika hali hiyo na Paul ni mazoea mabaya. Utani mwingi na kukosekana mipaka kati yetu, nilijisikia kusema chochote bila kumhofia, naye ilikuwa vilevile. Nilimshika nilipotaka bila hofu, nikawa natamani naye awe ananishika maeneo yenye shari.


“Ni mazoea hayo hayo yalinifanya nimpende Paul, hisia za kumpenda zilipoanza ndipo nikajikuta navutiwa na mavazi yake, u-handsome wake na kadhalika. Labda nigusie kitu kwamba kutoka na jinsi Paul alivyokuwa ananikosha, kuna tisheti yake moja niliipenda sana.
 
“Niliing’ang’ania anipe mpaka akanipa. Hiyo tisheti naipenda sana, ikawa kila mchana pale Paul akiwa kazini kwake, mimi nikimkumbuka naivaa. Ikazidi kuniweka karibu naye. Ukafika wakati nikawa najidanganya kwamba siwezi kuishi bila Paul.

0 comments:

Post a Comment