Monday, June 30, 2014

Msajili wa vyama vya Siasa amzuia Mbowe kugombea tena uenyekiti CHADEMA

By on 1:51 PM

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.
“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo

Aibu! Mwanamke amnasa KIKONGWE anayemtuhumu kumweka mwanaye ‘MSUKULE’ huko Mbagala

By on 7:08 AM

ULOZI! Katika hali ya kushangaza, mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika kwa jina moja la Siberi akiwa na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili lililotikisa, akimtuhumu kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara ‘msukule’.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina wakimhusisha kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.
Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
...Hii ni nyumba ya kikongwe huyo iliyoko maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar.
…Hii ni nyumba ya kikongwe huyo iliyoko maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini Dar.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.

CREDIT:GPL
  <<<KWA HABARI KILA SIKU BFYA HAPA ULIKE PAGE>>

Ndoa yawa Ndoano…Ndoa ya 3 ya DIDA yavunjika…!

By on 7:07 AM

KIMENUKA! Siku chache kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza, ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne inadaiwa kuvunjika, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuiripoti.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kililinyaka tukio zima nyumbani kwa mtangazaji huyo Mwananyamala-Manjunju, Dar, ishu hiyo ilijiri wiki iliyopita usiku ambapo majirani walimsikia Dida akilia lakini wakashindwa kutoa msaada kutokana na geti kufungwa.
“Tuligonga sana mlango lakini hakuna chochote ila baada ya muda tulimuona mume wa Dida akitoka nje na begi kisha akaingia kwenye Bajaj  na kuondoka, tukagundua walikuwa kwenye ugomvi,” kilisema chanzo hicho.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu โ€˜Didaโ€™ na mumewe, Ezden Jumanne anayepiga mzigo TV1 wakati wa harusi yao.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe, Ezden Jumanne anayepiga mzigo TV1 wakati wa harusi yao.

TATIZO NI NINI?

Chanzo kingine makini kimepenyeza madai kuwa ugomvi wa wawili hao uliibuka mara baada ya Ezden kuhoji juu ya mapato ya mkewe.
“Jamaa alikuwa anahoji mshahara na fedha ambazo mkewe anazipata katika shughuli za u-MC, alihoji pia kuhusu mwanaye kusoma Shule ya Saint Kayumba (hali ya chini) ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema chanzo hicho.

EZDEN AENDEWA HEWANI

Baada ya kunyetishiwa ishu nzima, mwanahabari wetu, alimtafuta Ezden kwa njia ya simu na kumsomea madai hayo ambapo hakuwa tayari kufafanua zaidi, alijibu kwa kifupi:
“Elewa tu kwamba tupo kwenye matatizo na mke wangu ila kwa sasa siko tayari kulizungumzia.
Bw. Ezden Jumanne akipozi.
Bw. Ezden Jumanne akipozi.

DIDA ANASEMAJE?

Kama ilivyo ada ili kupata uzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Dida, alipopatikana, alifunguka:
“Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa (Ezden) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri (pasword) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa, nikamuomba anifungulie, huwezi amini akaanza kunitukana, nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine!”

KIPIGO KINAENDELEA

Akiendelea kusimulia, Dida alisema ghafla, Ezden alichukua mkanda na kuanza kumpiga.
“Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji,” alisema Dida.

EZDEN ATIMKA

Chanzo kilidai kuwa, baada ya Ezden kuona amemuumiza mkewe, alikusanya nguo zake na kukimbia kwa usafiri wa Bajaj kwani Dida alificha funguo zote za magari yake.
“Alijua Dida atakwenda polisi hivyo akaona bora atimke zake,”  kilisema chanzo.

DIDA ATAKA TALAKA

Katika kuonyesha kuwa amechukizwa na tukio hilo la kupigwa ambalo amedai limekuwa likitokea mara kwa mara pamoja na kukosa imani naye katika masuala ya kuchepuka, Dida amesema kwa kuwa alishindwa kumuomba msamaha siku ileile ya tukio, anachotaka kutoka kwake ni talaka tu.
Khadija Shaibu โ€˜Didaโ€™.
Khadija Shaibu ‘Dida’.

TUJIKUMBUSHE

Tukio la kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwaka jana (siku tano kabla ya Mwezi wa Ramadhani kuanza) likikamilika kwa talaka, Dida atakuwa ametimiza idadi ya ndoa tatu kuvunjika.
Awali aliolewa na Mohamed Mchopanga ‘Mchops’ kisha Gervas Mbwiga ‘G’ na wote walimmwaga kwa talaka.
  <<<KWA HABARI KILA SIKU BFYA HAPA ULIKE PAGE>>

Dereva adai kuvunjwa Mkono na Askari Polisi huko Mbezi, Kimara jijini Dar.

By on 7:05 AM

DEREVA mmoja wa basi la Princes Muna linalofanya safari zalke toka Mwanza-Dar, Bw. Hamidu Juma anadai kupigwa na Polisi Juni 26 mwaka huu huko Mbezi, Kimara jijini Dar.
Akizungumza na mwandishi wetu, Hamidu alisema “Basi letu lina madereva wawili, zamu yangu ilikuwa imeisha, tulipofika Kimara tulikuta foleni, nikaamua kushuka ili kutazama sababu ni nini, niliporudi nikakuta basi letu liko pembeni likiwa limezungukwa na askari, baadhi wakiwa na nguo za kawaida, walitaka kung’oa karatasi za bima na zinginezo nikakataa ndipo wakadai nawafundisha kazi, wakaanza kunipiga mpaka mifupa ya mkononi imepishana’’.
DEREVA
Aidha dereva huyo anadai hajavunjika ila mifupa imepishana na pia ana uvimbe kwa hiyo amepewa siku saba ndipo arudi kufanyia uchunguzi wa kina.

UKATILI! Mwanamke auawa kwa wivu wa mapenzi huko Mpanda

By on 7:03 AM

MWANAMKE mmoja   aliyefahamika kuwa ni Cesilia  Clementi (22) Mkazi wa Mtaa wa Majengo B Mjini Mpanda ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Kanu ambaye ni mfanyabiashara wa Mpunga  wa kutoka mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Kamanda polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, tukio hilo la mauaji ya kusikikisha ya mwanamke huyo limetokea hapo jana  saa mbili asubuhi nyumbani  kwa  shemeji ya marehemu aitwaye Mashaka Hanja  katika Mtaa  huo wa majengo mjini hapa
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo marehemu ambaye alikuwa akiishi kwa dada yake mke wa Mashaka Hanja  walikuwa wanamahusiano ya  kimapenzi  na mpangaji wa nyumba hiyo, ambapo  aliamka asubuhi na kuanza kufagia nje ya nyumba hiyo.
Wakati akiwa anaendelea kufagia ndipo Kanu alitoka ndani na kumwita mpenzi wake huyo na kisha waliingia ndani ya chumba alichokuwa wakiishi ghafla majirani walianza kusikia marehemu akishutumiwa na  Kanu kuwa siku hizi hamjali kwa kuwa ameisha  pata mwanaume mwingine.
Walieleza  baada ya mabishano ya muda mfupi walisikia  marehemu akipiga mayowe   ya kuomba msaada na majirani hao walipojaribu kufungua mlango  walishindwa kwani ulikuwa umefungwa kwa ndani
Aliongeza kuwa majirani hao walijaribu kumsihi Kanu afungue mlango lakini hakufanya hivyo   hali ambayo iliwalazimu wachungulie dirishani na  kumwaona Kanu akimchoma marehemu na  kisu  kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.
Polisi walipata taarifa hizo    na mara walifika kwenye eneo hilo huku wakiwa na silaha na kuweza kuvunja mlango na walipoingia ndani walikuta marehemu akiwa ameishafariki dunia huku mwili wake ukiwa unagalagala chini ya sakafu
Na Kanu akiwa hoi huku na hana fahamu baada ya kuona amemuua mpenzi wake na yeye kuamua  kujichoma kisu katika sehemu ya tumbo  na shingoni
Jeshi la polisi   Mkoa wa Katavi limethibitisha kutokea kwa mauaji ya mwanamke huyo na wanamshikilia mtuhumiwa huyo huku akiwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  

Aibu! Vunja Jungu yamtokea Puani Njemba…Anaswa akila URODA na Mke wa Mpangaji wake GESTI

By on 7:01 AM


Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.
Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake.
OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.
Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali  akihusishwa  kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.
Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali akihusishwa kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa msimamizi wa gesti hiyo kufuatia  baba mwenye nyumba huyo kukahidi kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani na mzee huyo.
Walidai kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.
Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.
Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.
Ilidaiwa kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa  akimtaka mke wake kimapenzi.
Mke aliyekuwa akisumbuliwa, na ndugu wa mume wenye hasira wakizidi kumuadabisha mtuhumiwa.
Mke aliyekuwa akisumbuliwa, na ndugu wa mume wenye hasira wakizidi kumuadabisha mtuhumiwa.
Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
Baba mwenye nyumba akizidi kuchezea kichapo.
Baba mwenye nyumba akizidi kuchezea kichapo.

“Nilimwambia mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume huyo.
Baada ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.
Shauri hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji. Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.
CREDIT: GPL
               <<<KWA HABARI KILA SIKU BFYA HAPA ULIKE PAGE>>

Sunday, June 29, 2014

JWTZ sasa kulinda Amani mataifa ya Nje

By on 8:00 AM

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano wa ulinzi na amani katika mataifa yenye matatizo ya amani.
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam jana, wakati akizindua Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi na Amani, kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya Canada na kulenga kutoa mafunzo maalumu kwa maofisa wa Jeshi wa kulinda amani katika nchi zenye matatizo ya amani. Alisema mafunzo yatakayotolewa na chuo hicho yatasaidia kupunguza madhara ya ushambuliwaji wa wanajeshi watakaoshiriki katika ulinzi wa kulinda amani katika mataifa hayo.
“Chuo hicho kitakuwa kikipokea wanafunzi watakaopata mafunzo haya kutoka nchi mbalimbali zilizopo katika Jumuiya ya Kimataifa, zikiwemo Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Darfur – Sudan, ambazo tumekuwa tukishiriki kupeleka wanajeshi wetu wa kulinda amani na usalama katika mataifa yao. “Mafunzo yatakayotolewa katika chuo hicho yatahusiana na mbinu zote za kiusalama na amani kwa wanajeshi wa kulinda amani, ambao watakuwa wakijifunza jinsi ya kukabiliana na hatari pindi wawapo katika majukumu yao.
JWTZ
“Kutokana na mafunzo watakayoyapata, tunaamini hata madhara ya wanajeshi wetu waliokuwa wakienda kulinda katika nchi hizo yatapungua, kwani watakuwa na ujuzi zaidi, ikiwa ni pamoja na mbinu za kujilinda dhidi ya adui,” alisema Dk. Mwinyi. Alisema kutokana na uwepo wa chuo hicho nchini, amewataka wanajeshi wa kulinda amani kuitumia fursa hiyo katika kujiimarisha kimbinu na fikra ili waweze kupata uzoefu wa kutosha kabla ya kuingia eneo la vita.
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema wakufunzi wa mafunzo yatakayotolewa watatoka hapa nchini pamoja na baadhi ya mataifa rafiki wanaoshirikiana kutoa ulinzi na amani katika mataifa hayo. Alisema chuo hicho kimelenga kuanza kuchukua wanafunzi 70 watakaojifunza mafunzo hayo kulingana na aina ya masomo watakayochukua. Alisema katika kuepusha mwingilianao baina ya wananchi na chuo hicho, Jeshi limekusudia kuanza ujenzi wa wigo utakaowatenganisha ili kuepusha migogoro ya mwingiliano wa ardhi.
“Nawaomba wote watakaopata nafasi ya kujifunza mafunzo haya wawe makini na kutumia fursa hii katika kujiimarisha kimbinu, kwani itawasaidia pindi watakapokuwa katika eneo hatarishi kuweza kuchukua uamuzi sahihi wa kukabiliana na adui,” alisema Jenerali Mwamunyange.

NAFASI ZA KAZI MUHIMBILI HOSPITAL.... Procurement and Supplies Officer II - 1 Post

By on 7:49 AM
POSITION DESCRIPTION:

From The Daily News of 26th June
Muhimbili University of Health and Allied Sciences is inviting applications from suitably qualified Tanzanians to be considered for employment to fill the following vacant posts:-
Procurement and Supplies Officer II - 1 Post
Required Qualification
Holder of first degree/ advanced Diploma / Professional Level IV in
Materials Management or Procurement and logistics Management or its equivalent.


Required Qualifications
Holder of Master degree in Civil Engineering or Architecture plus five -t-
(5) years working experience in similar position and must have been registered by relevant Professional boards as practitioners.

Duties and Responsibilities
Provides specialized advice and service to the Directorate of Estates.
Formulates policies for Estates Management.
Develops objectives and plans, and installing Systems and procedures relating to Estates Management.
Participates in the development and implementation of training programmes for estates staff.
Provides consultancy service in Estates Management.
Makes feasibility studies and evaluates the viability of proposed projects in Estates Management.
Maintains co-coordinative work contacts with building staff or the Estates Development.
i) Takes prompt corrective action on any MUHAS infrastructure and
performing the Monitoring and Evaluation of Reports and ensures adherence to national and international operating standards.
Ensures that maintenance services are provided in accordance with international health standards, regulations and equipment methods of investigations.
Ensures that staff under the unit receives regular supervision and support in carrying out their duties.
) Enforces building rules and Municipal bylaws.
I) Takes full responsibility for supervising contractual building works undertaken by the University
ii) Plans, coordinates, controls and supervises maintenance of the University premises building and equipments.
v) Responsible for contract Management for works/construction.
I) coordinates the preparation of the physical master plan.
ri) Prepares annual budget estimates for repair of infrastructure and capital Development projects.
Iii) Performs any other duties as may be assigned by one's reporting officer.
Salary Scale PGSS 16-17


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Applicants must attach an up to date current Curriculum Vitae (CV) having reliable contact postal address, email address and telephone numbers.
The title of the position applied for should be written in the subject of the application letter and marked on the envelope.
Applicants must attach their detailed relevant certified copies of Academic certificates/transcripts
Form IV and Form VI result slips are strictly not accepted. Presentation of forged academic certificates and other information in the CV will necessitate to legal action.
Applicants currently employed in the public service should route their application letters through their respective employers.
Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts.
Certificates from foreign Universities should be verified by Tanzania Commission for Universities (TCU) or National Accreditation Council for Technical Education (NACTE) for foreign non degree certificates
Only shortlisted candidates will be informed the date for interview.
APPLICATION LETTERS SHOULD BE POSTED / HAND DELIVERED TO THE FOLLOWING ADDRESS on or before 4.00 pm on 8th July, 2014 (i.e, Deadline for receiving applications)
THE DEPUTY VICE CHANCELLOR, PLANNING, FINANCE AND ADMINISTRATION, MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES - MUHAS,
P.O. BOX 65001,
DAR ES SALAAM.


if you are qualified for this position
Please Follow the Application Instructions

     <<HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>