Sunday, July 6, 2014

BAADA YA KUNASWA KWA BABA MWENYENYUMBA KWA FUMANIZI:MUME AHAMA NYUMBA NA MKEWE KUMKIMBIA BABA MWENYE NYUMBA...PICHA ZA KILICHOTOKEA

By on 11:06 PM
Yule jamaa aliyefahamika kwa jina la Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akitaka kuvunja amri ya sita na mkewe, hatimaye ameamua kuhama nyumba.
...Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa fumanizi.
Fumanizi hilo liliripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari, ‘VUNJA JUNGU GESTI’ ambapo Huruma alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni, Dar.

Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.
Katika tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa na chanzo chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye nyumba huyo ili kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.

...Mke na mume walifunga virago vyote tayari kwa kuhama.
Wanahabari wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe wakibeba vitu ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.

...Mke na mume wakiwa nje ya nyumba waliyopanga.
“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma. 

...Mke na mume hao wakiondoka.
Alisema kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa umalizike Machi Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na bifu kubwa kiasi cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.
Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi jamaa huyo alidai alitekwa.

0 comments:

Post a Comment