Sunday, July 6, 2014

WAKANDARASI WA OVYO OVYO HATARINI MBIONI KUFUTIWA LESENI MKOANI NJOMBE

By on 4:40 AM



Jitihada za ujenzi wa barabara ya Ludewa Lupingu zikiendelea.
 
Serikali Imesema Itawafuta Kazi Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi ya Ujenzi Chini ya Kiwango Huku Ikiwaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Kuwasilisha Majina  ya Wakandarasi Wazembe Ili Hatua za Kisheria Zichukuliwa Dhidi Yao.

Kauli Hiyo Imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge Kwenye Kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Njombe Baada ya Wajumbe wa Kikao Hicho Kumlalamikia Mkandarasi wa Kampuni ya Nandra  Kuendelea Kujenga Barabara  za Lami  Chini ya Kiwango Mkoani Hapa.

Naibu Waziri Huyo wa Ujenzi Amewataka Mameneja wa Wakala wa Barabara Kote Nchini Kusimamia Kwa Karibu Miradi ya Barabara  Inayoendelea  Kujengwa na  Kubaini Wakandarasi  Wanaofanya  Kazi  Chini ya  Kiwango  Ili  Serikali  Ifutwa Katika Orodha ya Makandarasi Nchini.

Akizungumzia Kuhusu  Ujenzi wa  Daraja Katika Mto  Ruhuhu  Linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma Naibu Waziri  Lwenge Amesema Daraja Hilo Linatarajiwa Kujengwa Hivi Karibuni na Kurahisisha Miundombinu ya Mawailiano Baina ya Wananchi wa Maeneo Hayo

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kikao Hicho Keptein Mstaafu Aseri Msangi Ambaye Pia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ameagiza Kuitwa Mkandarasi  Huyo Anayelalamikiwa wa Kampuni ya Nandra  Ili  Kueleza  Sababu za  Kuendelea  Kufanya Kazi  Chini ya Kiwango Licha ya  Kuendelea  Kupewa Kazi  Huku Akiutahadharisha Uongozi wa TANROADS Mkoa Kuwajibika Juu ya Suala Hilo.

Awali Baadhi ya Wajumbe wa Kikao Hicho Wakiongozwa na Mbunge wa Makete Dkt. Binelithi Mahenge Wamesema ni Vema Serikali Mkoani Njombe na Wakala wa Barabara Mkoa Kuwa Makini na Mkandarasi Huyo Kutokana na Kushindwa Kutekeleza Miradi ya Ujenzi Kwa Wakati na Kiwango Kinachotakiwa Huku Akitolea Mfano Barabara Wilayani Makete Yenye Urefu wa Kilomita 1.5 Ambayo Ametekeleza Kwa Asilimia 10 Tu.
 
Na Gabriel Kilamlya

0 comments:

Post a Comment