Saturday, July 5, 2014

Utafiti: Wapenzi wanaotumia muda mwingi Twitter hupoteza uaminifu na kuvunja uhusiano wao

By on 8:50 PM
the QUARTZ Blog

Mitandao ya kijamii ina madhara hasi na madhara chanya kwa watu walio katika uhusiano wa mapenzi. Lakini tafiti zinaonesha kuwa mitandao hii huwa na madhara hasi zaidi kwenye uhusiano kuliko madhara chanya (faida).
Mwaka jana kulikuwa na ripoti za tafiti mbalimbali zilizooonesha kuwa Facebook huchangia kwa kiasi kikubwa kuvunja uhusiano lakini mwaka huu utafiti mpa unaonesha kuwa mtandao wa Twitter unahusika kuvunja uhusiano wa mapenzi kwa kiasi kikubwa kwa wapenzi wanaotumia muda wao mwingi kutweet.
Utafiti uliofanywa na Russell Clayton ambaye ni  mwanafunzi anaechukua Phd (Uzamivu) wa chuo kikuu cha Missouri-Columbia, unaonesha kuwa couple zinazotumia muda mwingi ku-tweet huzua malumbano, mabishano, wivu na mwisho wake huvunjika.
Utafiti huo unaonesha kuwa kadri couple zinavyozidi kuwa ‘active’ kwenye mitandao ya kijamii ndivyo ambavyo uhusiano wao unakuwa katika hatari ya kuvunjika.
Katika utafiti huo, Russell alipima muda ambao watu walio katika uhusiano wanatumia katika Twitter, mabishano au ugomvi unaozuka kati yao kutokana na matumizi hayo matokeo yake kwa uhusiano wao.

Mtafiti huyo alieleza Journal ya Cyberpsychology, Behaviour and Social Networking kuhusu maelezo yake maelezo haya:
“Active users of social networking who are in a romantic relationship may find that Twitter-related conflicts cause relationship problems that can become serious enough to result in infidelity or divorce.The length of the romantic relationship does not alter the findings so that even long married couples can fall out over Twitter as much as newlyweds.”
 

0 comments:

Post a Comment