Saturday, July 5, 2014

WEMA akimbilia TCRA kumsaka mtu aliyetengeneza Picha Chafu ya Mama yake Mzazi

By on 8:45 PM

Miss  Tanzania  2006/2007  Wema  Sepetu  ameiomba  Wizara  ya  Sayansi  na  Teknolojia  kupitia  Mamlaka  ya  Mawasiliano  Tanzania  ( TCRA )   kumsaka  mtu  aliyetengeneza  picha   chafu  ya    mama  yake  mzazi, Mariam  Sepetu  na  kisha  kuisambaza  kwenye  mitandao  ya  kijamii……
wema
 
Akizungumza  na  mwanahabari  wetu, Wema  alisema  anaamini  kuwa  TCRA  wanao  uwezo   wa  kumbaini  mtu  huyo  ambaye  bado  hajamfahamu  ili  sheria  iweze  kuchukua  mkondo  wake  kwani  amemdhalilisha  mzazi  wake  bila  sababu  yoyote….
 
“Nafanya  utaratibu  wa  kwenda  TCRA  ili  wamsake  aliyefanya  kitendo  hicho  kwani  uwezo   huo  wanao,” alisema  Wema
mama wema
Mama Wema


Mrembo  huyo  alisema  serikali  isisubiri  mpaka  tukio  hilo  limkute  kiongozi  wa  serikali  ndo  waanze  kuhaha  kwani  tabia  hiyo  inaonekana  kuota  mizizi  baada  ya  hivi  karibuni  kufanyiwa  hivyo  wabunge.

0 comments:

Post a Comment