Saturday, July 5, 2014

Wizara ya Afya yawanyooshea kidole Madaktari Feki

By on 8:48 PM

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania imewaonya watu wanaojiita madaktari na maprofesa bila ya kuwa na sifa hizo huku wakidai kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa yasiyotibika ukiwemo ugonjwa wa Ukimwi na kisukari.
 
Mganga mkuu wa serikali Dkt Donnan Mmbando ametoa onyo hilo jijini Dar es Salaam jana, na kufafanua kuwa wenye haki ya kujiita hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia tiba asili na tiba mbadala nchini Tanzania, ni wale tu wenye sifa zinazotambulika na mamlaka mbalimbali za serikali. Dkt Mmbando amesema inashangaza kuona watu wakijitangaza na kujinadi eti ni madaktari na wana uwezo wa kutibu magonjwa hayo na mengine ambayo yameshindikana ilhali sio kweli bali ni njia za kijanja za kutaka kujipatia pesa.
Aidha, Dkt Mmbando amesema katika kuhakikisha dawa za tiba asili na tiba mbadala zinatolewa kwa mujibu wa viwango vinavyotambulika kisheria, wizara inakamilisha taratibu kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa na jukumu la kusindika dawa zote za asili ili ziwe katika mwonekano na viwango vya kisasa. 
maganga Usindikaji huo kwa mujibu wa Dkt Mmbando, utafanana na dawa zinazotumiwa katika hospitali na vituo vya huduma za kisasa, hatua itakayowafanya wananchi waachane na kuchemsha mizizi na kunywa katika hali ambayo hairidhishi kiafya.

0 comments:

Post a Comment