- Mnyika asema Katiba ya Chadema ya 2006 haikurekebishwa, bali iliundwa upya
- Jaji Mutungi asema ofisi yake inafanya kazi kitaaluma na haiingizi siasa
Pia, chama hicho kimemtaka Jaji Mutungi ajitokeze hadharani
kubainisha iwapo yeye ndiye aliyemtuma msaidizi wake, Sistyl Nyahoza
kutangaza kuwa mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk
Willibrod Slaa hawana sifa ya kugombea uongozi ndani ya chama hicho
kutokana na kuzuiwa na katiba ya Chadema.
Jana, Nyahoza alikaririwa na vyombo vya habari akisema Mbowe na Dk
Slaa hawana sifa za kugombea uongozi wa chama hicho kutokana na katiba
ya chama chao kuwabana.
Alibanisha kuwa kipengele cha ukomo wa mgombea katika katiba yao ya
mwaka 2006 kiliondolewa kinyemela bila idhini ya mkutano mkuu.
Nyahoza alisema katiba ya Chadema ya mwaka 2004, ilikuwa na kipengele
cha ukomo wa madaraka kuwa kiongozi aliyeongoza vipindi viwili vya
miaka mitano mitano, hawezi kuwania tena nafasi hiyo.
Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema
Jaji Mutungi hana mamlaka ya kubaini sifa za viongozi wa chama hicho,
bali wenye mamlaka hayo ni wanachama wa chama hicho pekee.
Mnyika alisema mwaka 2006, katiba ya Chadema haikurekebishwa, bali
iliundwa upya na kuridhiwa na mkutano mkuu wa chama na kwamba Agosti 13,
2006 ilizinduliwa na nyaraka zote alikabidhiwa Msajili wa Vyama wa
wakati huo, John Tendwa.
Katika uzinduzi huo wa katiba pamoja na bendera mpya ya Chadema,
Tendwa alikimwagia sifa chama hicho kwa kuonyesha mwelekeo na mwenendo
mzuri na kuvishauri vyama vingine viungane nacho kuunda chama cha
upinzani chenye nguvu nchini.
Akizungumzia mabadiliko hayo, Mbowe alikaririwa na gazeti hili Agosti
15, 2013 akisema yalikuwa yanalenga kuimarisha mapambano ya kisiasa ya
chama hicho.
Mnyika alisema: “Mkutano mkuu wa
chama uliipitisha Katiba hiyo baada ya mchakato mrefu wa kukusanya
maoni kutoka kwa mabaraza ya wilaya na majimbo. Hatukurekebisha katiba
kama inavyoidaiwa. Ni makubaliano ya wanachama wote ambao waliafikiana
na mambo yaliyotakiwa kuwamo.”
Alisema katika mchakato huo kulikuwa na makubaliano na mabishano
katika baadhi ya masuala lakini suala la ukomo wa uongozi liliafikiwa na
wanachama wote bila tatizo na kupitishwa kuingia katika katiba na Ofisi
ya Msajili ilipelekewa fomu ya marekebisho pamoja na katiba mpya kama
sheria inavyotaka… “Kama wameipoteza waseme tuwapatie katiba wairejee.”
“Tunachomtaka Mutungi ni
kuheshimu katiba ya chama na kuwaheshimu wanachama wa Chadema na
ayapuuze madai ya wasaliti wachache. Kama vipi asubiri aone uamuzi wa
Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ubainishe kama katiba ilivunjwa,” alisema Mnyika.
Mnyika alisema wameshtushwa na kauli ya ofisi hiyo na kuituhumu kwamba imeanza kutumika kisiasa na wasaliti.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo jana, Jaji Mtungi alisema:
“Hili suala lisimamiwe na chama husika kwa kuwasiliana na Ofisi ya
Msajili… hakuna haja ya kulikuza katika vyombo vya habari. Wanachama wa
Chadema watapata taarifa kutoka kwa viongozi wao ni nini kinaendelea.”
Kuhusu madai kwamba ofisi yake inatumika kisiasa alisema: “Kama
nilivyosema, hayo tuyaache hii ofisi yetu ipo more technical (kitaalamu
zaidi) hatuingizi siasa. Wao (Chadema) waje kwenye ofisi yetu tuongee
kama taasisi, iwapo tunataka kuwasilisha jambo katika vyombo vya habari,
basi tutaitisha mkutano na waandishi wa habari,” alisema Mutungi.
Mamlaka ya msajili
Mnyika aligusia pia mamlaka ya msajili huyo akisema… “Hana
mamlaka ya kutangaza sifa za mgombea wa Chadema. Sifa na uamuzi
vimetajwa katika katiba na kanuni za chama. Kifungu cha 6.3.2 cha katiba
ya 2006 kinabainisha wazi kuwa kiongozi aliyemaliza muda wake na mwenye
sifa ya kugombea anaruhusiwa kugombea…?” Alisema hata katika
uchaguzi wa ndani wa mwaka 2009 viongozi wengi walichaguliwa na wakiwa
wameshamaliza ukomo wa uongozi na msajili wa vyama hakuzungumza
chochote.
Alisema hawababaishwi wala kuguswa na uamuzi uliotolewa na Ofisi ya
Msajili wa kwa kuwa mkutano mkuu wa Chadema unaotarajiwa kufanyika
baadaye mwaka huu, ndiyo utakaoamua hatima wa kiongozi yeyote wa chama
hicho.
0 comments:
Post a Comment