USHIRIKINA
umetajwa kwa mahabusu wa Gereza la Wilaya ya Geita waliovua nguo mbele
ya Mahakama ya Mwanzo ya Nyankumbu mkoani hapa wakimshinikiza Mkuu wa
Mkoa wa Geita (Said Magalula), Jaji Mkuu (Mohammed Chande Othman) na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Stephen Werema) kusikiliza madai yao ya
msingi.
Tukio
hilo lilijiri Juni 26, mwaka huu saa 3:00 asubuhi ikiwa ni muda mfupi
baada ya kutoka mahakamani bila kesi zao kusikilizwa na kutakiwa kupanda
kwenye gari la polisi kurudishwa mahabusu.
Wakati
sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walisikika wakisema kuna
uwezekano madai ya mahabusu hao si waliyoyasema bali ni imani za
kishirikina kutoka kwa waganga.
“Unaweza
kusema wanadai kusikilizwa, kumbe wanatumikia maelekezo ya waganga,
wengine wanaambiwa mkifika mahakamani vueni nguo, sasa watavuaje watu
wakawaelewa, si lazima wazue balaa la kutaka haki,” alisema mkazi mmoja wa Geita.
Iliendeelea
kudaiwa kuwa, wapo mahabusu wengi wanaofanya matendo ya kuashiria
ushirikina kwa sababu katika hali ya kawaida, si rahisi mtu timamu kuvua
nguo, wengi hutumia njia ya kugoma kula.
“Tunataka
haki, tumechoka kuonewa, watu tunasingiziwa kesi za mauaji, wengine
tuna kesi za wizi lakini kila siku kesi zinaahirishwa kwa madai eti
hakuna ushahidi, tumefika hapa leo tunaambiwa kesi zimeahirishwa,” walisikika wakisema mahabusu hao.
Mahabusu
hao pia waligoma kuingia kwenye gari la polisi na kubaki
wakiung’ang’ania mlingoti wa bendera ya taifa iliyo mbele ya mahakama
hiyo huku wakisema endapo wangepigwa wangeing’oa bendera hiyo.
“Vaeni nguo, mkuu wa mkoa hawezi kuja kuongea na watu mkiwa uchi hivi halafu mpande kwenye gari twende gerezani tukazungumze,” alisema kaimu ofisa usalama wa Mkoa wa Geita ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Mahabusu
hao walikubali kuvaa nguo lakini wakaendelea na mgomo wa kuingia kwenye
gari, muda mfupi alifika Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Gasper
Kanyaita kuzumgumza nao kwa niaba ya mkuu wa wilaya ndipo wakakubali
kuingia kwenye gari la polisi lenye namba za usajili PT 1166.
0 comments:
Post a Comment