Daniel
Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria
katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha
University College – RUCO), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kisha
kuchomwa moto na wananchi wenye hasira akidhaniwa kuwa mwizi.
Tukio
hilo lilitokea Juni 24, 2014, majira ya saa 5 usiku ambapo inadaiwa
kuwa Daniel alikuwa ametoka kuangalia michuano ya Kombe la Dunia, akawa
anatafuta chakula cha jioni ambapo alipofika kwenye mgahawa mmoja ambao
ulikuwa umefungwa, aliingia ndani ambapo binti aliyekuwa amelala ndani
ya mgahawa huo, alianza kupiga kelele za mwizi zilizowakusanya wananchi
wenye hasira kali.
Wananchi
hao walianza kumshambulia Daniel wakiongozwa na mlinzi mmoja wa jamii
ya Kimasai, baada ya kuzidiwa na kichapo wananchi hao walimmwagia mafuta
ya taa na kumchoma moto kisha wote wakatoweka.
Mwanafunzi
huyo aliokolewa na madereva bodaboda ambao walizima moto na kumkimbiza
katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa lakini siku kadhaa baadaye alifariki
dunia.
Mwili
wa marehemu umeagwa mapema leo katika hospitali hiyo tayari kwa safari
ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika
kesho Jumatano.
Daniel
Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria
katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha
University College – RUCO) enzi za uhai wake.Credit: Habari leo
0 comments:
Post a Comment